Karibu kwenye Blog ya Kijamii ya Kigoma yetu kwa habari na matangazo kwa bei nafuu sana. Tunakalibisha maoni, ushauri na habari zako ili tuijenge Tanzania kwa pamoja.

Tuesday, April 30, 2013

Mwanafunzi ashinda mil.100/- za Vodacom Kigoma

MWANAFUNZI wa Chuo cha Ualimu Kigoma, Valerian Nicodemus (22) ameshinda Sh milioni 100 za promosheni iliyokuwa ikiendeshwa na Kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom. 

Nicodemus ameibuka mshindi wa jumla wa promosheni hiyo baada ya kuchezeshwa kwa droo kubwa iliyoshirikisha mamilioni ya washiriki, ambao ni wateja wa kampuni hiyo ya simu.
Akizungumzia ushindi, Nicodemus alisema hakutarajia maishani mwake kupata kiasi kikubwa cha fedha kama hicho.

Sikuwa na pesa ya kucheza moja kwa moja katika Promosheni hii ila nilipotumiwa pesa ya matumizi na Mzee niliamua kuweka na kushiriki katika Promosheni hii, hakika nimefurahi sana na ninawashukuru Vodacom,” alisema.

Aliendelea kusema, “Awali sikuwa naamini kabisa kama kweli mtu anaweza kushinda kihalali, yalikuwa mawazo potofu, lakini kweli yametokea na ninamshukuru Mungu na pia Vodacom kwa kuyabadilisha kabisa maisha yangu”.

Mkuu wa Kitengo cha Masoko na Mawasiliano wa Vodacom Tanzania, Kelvin Twissa amempongeza Nicodemus na washindi wengine.

Alisema anajivunia mafanikio ambayo promosheni hiyo imeyapata kwa kubadili maisha ya mamia ya Watanzania.
Tangu kuanza kwa promosheni hiyo Januari 24 mwaka huu, washindi 333 wamepatikana na kugawana zaidi ya Sh milioni 480 zilizokuwa zinashindaniwa na washindi kupatikana kila siku, kwa wiki na hatimaye droo kubwa iliyompa ushindi Nicodemus.

No comments: