Karibu kwenye Blog ya Kijamii ya Kigoma yetu kwa habari na matangazo kwa bei nafuu sana. Tunakalibisha maoni, ushauri na habari zako ili tuijenge Tanzania kwa pamoja.

Tuesday, April 30, 2013

Zitto apongeza Serikali kujenga Daraja Malagarasi




Kabwe Zitto

NAIBU Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Kabwe Zitto amepongeza Serikali kukamilisha ujenzi wa barabara ya kiwango cha lami kutoka Kigoma hadi Uvinza na kukamilika kwa Daraja la Malagarasi.

Zitto alitoa pongezi hizo kwenye mkutano wa hadhara wa chama chake uliofanyika mjini Tabora.
Pia, katika mkutano huo, aliwahimiza wananchi wa Tabora kupata mbunge kutoka Chadema, kwa kile alichodai kuwa bila kufanya hivyo, hawatapata barabara za lami.

Alisema barabara ya kutoka Uvinza kwenda Tarafa ya Nguruka, Kigoma Vijijini inaendelea kukamilishwa kwa kiwango cha lami ili wananchi wa Kigoma waendelee kutumia kodi yao kikamilifu.

Alisema licha ya hayo yote, Serikali bado ina wajibu mkubwa kuhakikisha wananchi wa Tabora, pia wananufaika na miradi ya barabara kwa kiwango cha lami. Zitto alisema alipita njia ya kutoka Kigoma hadi Tabora Mjini kupitia Nguruka na Urambo na kujionea barabara ilivyo mbovu.

Alisema tatizo kubwa lililopo ni kuunganisha barabara hizo na mikoa mingine nchini.
Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe alisema jambo linalomkera ni uwepo wa utitiri wa vyama vingi nchini, ambavyo alidai vingi havijui mustakabali wa nchi.
Alisema utitiri huo, unasababisha upinzani kushindwa kukamata Dola na kukiondoa madarakani Chama Cha Mapinduzi (CCM).

No comments: