Karibu kwenye Blog ya Kijamii ya Kigoma yetu kwa habari na matangazo kwa bei nafuu sana. Tunakalibisha maoni, ushauri na habari zako ili tuijenge Tanzania kwa pamoja.

Wednesday, March 6, 2013

Kortini kwa tuhuma za kumchoma mtoto wa kambo

MFANYABIASHARA mkazi wa Manispaa ya Kigoma/Ujiji, Regina Alphonce (27) amefikishwa mahakamani na kusomewa shitaka la kumjeruhi kwa kumchoma moto mtoto wake wa kambo mwenye umri wa miaka saba.

Mwendesha Mashitaka wa Serikali, Athumani Mshana alidai mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama hiyo, David Ngunyale kuwa mshitakiwa alimchoma kwa moto na kumsababishia maumivu mtoto huyo, ambaye ni mtoto wa mumewe aliyezaa na mwanamke mwingine.

Mwendesha Mashitaka alidai mshitakiwa huyo alitenda kosa hilo kati ya Februari 20 na 23 mwaka huu saa 4 asubuhi katika eneo la Katubuka. Mtoto huyo ni mwanafunzi wa darasa la kwanza katika Shule ya Msingi Kiezya iliyopo Manispaa ya Kigoma/ Ujiji.

Mshitakiwa alikana kosa hilo na kudai kuwa ni utundu wa mtoto huyo. Hakimu Ngunyale aliahirisha kesi hiyo na kuamuru mshitakiwa arudishwe rumande hadi Machi 14 mwaka huu, kesi hiyo itakapotajwa tena mahakamani hapo.

No comments: