Kwa Waziri mwenye dhamana na wadau wote:
Huu ndio utaratibu unaotumika kukata tiketi za treni ya
abiria mkoani kigoma. ni utaratibu uliojaa udhalilishaji na hali zote zisizo za
kiubinadamu. foleni huwa ndefu sana na huuzwa
tiketi chache sana
na wananchi kutangaziwa kuwa zimekwisha. hivyo inawabidi watu kulala station
kigoma wakipigwa na baridi huku wakiliwa na mbu pia ili kuwahi foleni hiyo waweza
pata tiketi kihalali na kukamilisha safari zao. kinachosikitisha zaidi ni kuwa
tiketi hizo hizo huendelea kuuzwa nje kidogo ya ofisi za TRL kwa bei kubwa.
Imekuwa ni biashara ya Kawaida kabisa mkoani hapo.
tunahitaji utaratibu wa booking urudi ili kutoa fursa ya mtu kufika pale kwa
nafasi yake badala ya kupanga foleni ndefu ka watumwa sokoni. pili,
walanganguzi wa tiketi ukomeshwe mara moja. NATAMBUA kuwa mnaweza yakamilisha
hayo mkiamua...
Imetoka kwa Mdau John N Bakunda
No comments:
Post a Comment