Mganga Mkuu wa Mkoa Kigoma, Dr.Leonald Subi |
JUMLA ya watu 473 mkoani Kigoma wakiwemo wanaume 23
wamejitokeza kupatiwa huduma ya kufunga kikazi katika kipindi cha miezi mitatu
iliyopita ikiwa ni katika mkakati wa utekelezaji wa uzazi wa mpango na kufuata
nyota ya kijani.
Mganga Mkuu wa Mkoa Kigoma, Leonald Subi alisema hayo wakati
wa uzinduzi wa mradi wa huduma za mkoba za uzazi wa mpango na upimaji wa hiari
wa Virusi Vya Ukimwi .
Mganga huyo alisema kuwa kwa idadi hiyo ya watu hayo ni
mafanikio makubwa tangu kuanza kutekelezwa kwa mpango huo mwezi Julai mwaka huu
hasa kwa kuzingatia historia na utamaduni wa wananchi wa Mkoa Kigoma.
Subi alisema kuwa Mkoa wa Kigoma kwa miaka mingi umekuwa na
takwimu za juu za watoto wanaozaliwa huku familia nyingi za wananchi wa mkoa
huo wakiwa wanazaa bila kujali uzazi wa mpango jambo ambalo limechangia
umasikini kwa familia nyingi mkoani humo.
Awali Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu wa Marie Stops Tanzania,
Zawadi Athanas alisema kuwa uzinduzi wa mradi huo kwa Mkoa Kigoma na sehemu ya
utekelezaji wa mradi wa miaka minne kwa mikoa 26 ambayo itafikiwa na huduma hizo
za mkoba za uzazi wa mpango.
Akizindua mradi huo Mkuu wa Mkoa Kigoma, Issa Machibya
alitoa wito kwa jamii ya mkoa huo kufuata njia za uzazi wa mpango zilizokubaliwa
na wataalamu kwani kufanya hivyo kutasaidia kuinua uchumi wa familia nchini .
Mkuu huyo wa Mkoa alisema kuwa bado Mkoa Kigoma una takwimu
za chini za watu wanaojitokeza kufuata uzazi wa mpango na kueleza kushangazwa
na kuongezeka kwa takwimu za wanawake walioolewa kuendelea kushindwa kupata
huduma za uzazi wa mpango.
No comments:
Post a Comment