MKOA wa Kigoma bado unakabiliwa na changamoto kubwa ya
kuendelea kuwepo kwa vifo vya wajawazito na watoto chini ya miaka mitano
kutokana na wajawazito wengi kujifungulia nyumbani.
Mganga Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Dk
Leonard Sumbi alisema hayo wakati wa mkutano wa wadau wa Sekta ya Afya mkoani
humo uliokuwa ukijadili mkakati wa kupunguza vifo vya mama wajawazito na watoto
chini ya miaka mitano.
Dk Maginga alisema kuwa zaidi ya asilimia
42 ya wanawake wajawazito mkoani humo bado wanajifungulia majumbani na watoto
au wanawake hao hufariki dunia kutokana na kuchelewa kufikishwa hospitalini
wanapopatwa na matatizo wakati wa kujifungua.
Sambamba na hilo, alisema kuwa suala
la uchache wa watumishi katika Sekta ya Afya na miundombinu duni ya usafiri
katika maeneo ya mbali vijijini kufika katika maeneo ya utoaji huduma za afya
ni miongoni mwa changamoto zinazochangia katika ongezeko la vifo hivyo.
Hata hivyo, alisema kuwa kuanzishwa
kwa huduma za upasuaji katika vituo 12 vya afya mkoani humo kulikofanywa
kupitia ufadhili wa taasisi ya World Lung Foundation kumesaidia katika
kukabiliana na vifo vya wanawake wakati wa kujifungua kutokana na kufanyiwa
upasuaji mdogo kwenye vituo hivyo.
No comments:
Post a Comment