Karibu kwenye Blog ya Kijamii ya Kigoma yetu kwa habari na matangazo kwa bei nafuu sana. Tunakalibisha maoni, ushauri na habari zako ili tuijenge Tanzania kwa pamoja.

Saturday, August 25, 2012

Bonanza kuhamasisha sensa leo Kigoma

HALMASHAURI ya Manispaa ya Kigoma Ujiji inatarajia kuendesha bonanza la michezo litakalofanyika leo kwenye Viwanja vya Mwanga Community Centre mjini Kigoma likiwa na nia ya kuhamasisha Sensa ya Watu na Makazi inayotarajiwa kuanza Jumapili wiki hii.

Akizungumza mjini Kigoma na waandishi wa habari, Mkurugenzi wa Manispaa ya Kigoma Ujiji, Alfred Luanda amesema moja ya sababu kuu za kuwepo kwa bonanza hilo ni kuwapa nafasi watu ambao hawajapata elimu kuhusu sensa kupitia vyombo vya habari na maeneo mengine kupata ujumbe na kuweza kufanikisha shughuli hiyo.

Luanda amesema bonanza hilo litafanyika kwenye Viwanja vya Mwanga Community Centre mjini Kigoma mahali ambapo wadau na watu mbalimbali watafika kwa urahisi, lakini pia ni eneo ambalo lina msongamano mkubwa wa watu na ujumbe unaweza kusambaa kwa urahisi.

No comments: