Karibu kwenye Blog ya Kijamii ya Kigoma yetu kwa habari na matangazo kwa bei nafuu sana. Tunakalibisha maoni, ushauri na habari zako ili tuijenge Tanzania kwa pamoja.

Thursday, June 28, 2012

Wanafunzi wawili wafa kwa radi Kigoma

WATU watatu wakiwamo wanafunzi wawili wa shule ya msingi wilayani Kasulu na mkulima mmoja katika wilaya hiyo, wamefariki dunia kutokana na kupigwa na radi ambayo pia imejeruhi mtu mwingine.

Akizungumza mjini hapa na waandishi wa habari, Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kigoma, Fraiser Kashai aliwataja watu hao waliofariki kuwa ni Jackline Leonald mwanafunzi wa darasa la nne katika Shule ya Msingi Rusesa wilayani Kasulu na ndugu yake, Maria Leonald walikutwa na mauti wakiwa njiani kurejea nyumbani wakitokea shambani.

Kamanda alimtaja mwanafunzi mwingine aliyefariki katika tukio hilo kuwa ni Zuwena Cosmas wa Shule ya Msingi Kagera Nkanda ambapo pia radi hiyo ilimjeruhi Rahel Lucas (10) mkazi wa kijiji hicho cha Kagera Nkanda ambaye anapatiwa matibabu kwenye zahanati hiyo ya kijiji.

Kamanda Kashai alisema matukio hayo yaliyotokea saa nne asubuhi , yanatokana na mvua kubwa iliyokuwa ikinyesha katika maeneo hayo ambayo iliambatana na radi kubwa.

Katika tukio lingine, mfanyakazi wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) Mkoa wa Kigoma, Ally Mgaya amejeruhiwa kichwani kutokana na basi la abiria la Kimotco lililokuwa likifanya safari ya kutoka Kigoma kwenda Dar es Salaam kupinduka na ambapo abiria zaidi ya 20 walijeruhiwa.

Kamanda Kashai alisema ajali hiyo ilitokea eneo la Senga Gungu mjini Kigoma saa 12 asubuhi wakati basi hilo lenye namba za usajili T369 ASE aina ya Scania lililokuwa likiendeshwa na Mohamed Bakari lilipoacha njia na kugonga ukuta wa mtaro na kisha kutumbukia mtaroni.

Alisema baada ya ajali hiyo majeruhi hao walipatiwa matibabu na kuruhusiwa kurudi nyumbani ambapo abiria watatu wamelazwa hospitalini pamoja na askari


No comments: