Karibu kwenye Blog ya Kijamii ya Kigoma yetu kwa habari na matangazo kwa bei nafuu sana. Tunakalibisha maoni, ushauri na habari zako ili tuijenge Tanzania kwa pamoja.

Saturday, June 30, 2012

Kipimo cha malaria kusaidia kudhibiti unywaji dawa holela Kigoma



KIPIMO cha haraka cha kutambua malaria kimeelezewa kuwa kitasaidia kudhibiti matumizi ya dawa ambazo zilikuwa zikitolewa kwa watu waliokuwa wakidhaniwa wana ugonjwa huo wakati hawana kutokana na kutokuwepo na vipimo.

Mganga Mkuu wa Wilaya Kigoma, Edwin Kilimba alisema hayo wakati wa ufunguzi wa mafunzo kwa watoa huduma wa zahanati na vituo vya afya vya wilaya hiyo juu ya matumizi ya kipimo hicho yanayofanyika mjini hapa. Kilimba alisema kipimo kitasaidia kufahamu kwa uhakika kama mgonjwa aliyefika kwenye kituo cha afya ana malaria au la
Alisema sehemu kubwa ya zahanati katika wilaya hiyo hazina darubini ya kupimia malaria na hivyo watoa huduma hutumia mazoea kwa kuangalia dalili za ugonjwa huo na hivyo kufanya matumizi makubwa ya dawa ya Alu ambayo hulalamikiwa kwamba huwa zinachukua muda mfupi kuwepo kwenye zahanati.

Mwezeshaji wa mafunzo ya matumizi ya kifaa hicho kutoka Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Matilda Joseph alisema dawa za Alu zimekuwa na matumizi makubwa nchini kutokana na utoaji holela ikidhaniwa kuwa kila anayelalamikia maumivu ana malaria

No comments: