Karibu kwenye Blog ya Kijamii ya Kigoma yetu kwa habari na matangazo kwa bei nafuu sana. Tunakalibisha maoni, ushauri na habari zako ili tuijenge Tanzania kwa pamoja.

Thursday, June 28, 2012

Mchango wa Zitto Bungeni-Hotuba ya Waziri Mkuu: Haki za Uraia, Mafuta/Gesi Asilia na Uwajibikaji

 Haki za Uraia, Mafuta/Gesi Asilia na Uwajibikaji


Unyanyasi wa Watu wa Kigoma
Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru kwa kunipa fursa ya kuchangia Hotuba hii ya Waziri Mkuu. Jana Mheshimiwa Waziri amekuja kuomba Bunge limuidhinishie jumla ya shilingi trilioni 3.8 kwa ajili ya Ofisi yake na taasisi zote zilizo chini ya Ofisi yake pamoja na takribani shilingi bilioni 113 kwa ajili ya Bunge. Fedha zote hizi takribani shillingi trilioni 3.2 zinakwenda Wizara ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kabla hatujaweza kumuidhinishia Mheshimiwa Waziri Mkuu fedha hizi na yeye kama Mkuu wa Shughuli za Serikali, msimamizi wa kazi za Serikali za kila siku na ambaye anaangalia utendaji wa takribani Mawaziri, wote ni vizuri aweze kutoa majibu kwa baadhi ya masuala ambayo mengine ameyaainisha kwenye hotuba yake, lakini mengine hakuyaainisha katika hotuba yake.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nitaanza na Kigoma. Mheshimiwa Waziri Mkuu katika ukurasa wa 51 wa Hotuba yake amezungumzia masuala ya ulinzi na usalama lakini hakugusia kabisa operesheni ambazo zinaendelea hivi sasa katika Mkoa wa Kigoma nadhani na Mkoa wa Kagera kuhusiana na masuala ya wahamiaji haramu. Hivi tunavyozungumza ni kwamba mamia ya watu wa Kigoma wameonyeshwa kwamba siyo raia wa Tanzania. Utaratibu huu umekuwa ukiendelea mwaka hadi mwaka. Napenda Mheshimiwa Waziri Mkuu akumbuke historia baada ya Vita vya Kwanza vya Dunia kati ya mwaka 1918 na mwaka 1924 Kigoma haikuwa sehemu ya Tanganyika. Kigoma ilikuwa inatawala kama inavyotawaliwa tofauti sasa hivi Burundi kama inavyotawaliwa sasa tofauti Rwanda. Kwa muda mrefu sana Mkoa wa Kigoma umeachwa nyuma katika kila kitu eneo la maendeleo.
Mimi nimeona lami ya kwanza ya highway mwaka 2008. Miaka zaidi ya 40 baada ya uhuru. Leo hii watu wa Kigoma wa maeneo ya Kusini mwa Kigoma wa maeneo ya Kaskazini mwa Kigoma wanasombwa kwenye maboti, wanasomwa kwenye magari wakiambiwa kwamba siyo raia wa Tanzania. Hatuwaoni Wamakonde wakiambiwa kwamba siyo raia wa Tanzania na wanapakana na Msumbiji. Hatuwaoni Wamasai wanaambiwa siyo raia wa Tanzania na wanapakana na Kenya. Hatuwaoni Wachaga wanaambiwa siyo raia wa Tanzania wanapakana na Kenya. Hatuwaoni Wanyakyusa wanaambiwa siyo raia wa Tanzania wanapakana na Zambia na vile vile wanapakana na Malawi.
Kwa nini suala hili liwe ni kwa watu wa Kigoma na watu wa Katavi peke yake? Kwa nini tunatumia fedha za nchi, polisi wa nchi kwenda kusumbua watu wa Kigoma. Nilikuwa naomba Mheshimiwa Waziri Mkuu operesheni inaendelea sasa hivi katika Mkoa wa Kigoma kuwanyanyasa Raia wa Kigoma waonekane ni Raia wa Tanzania wa daraja B ikome mara moja na viongozi wa Kisiasa, Wabunge wote  wa Mkoa wa Kigoma na Wakuu wa Wilaya na Wakuu wa Mikoa tukae tuweze kuangalia kwa sababu kuna uonevu wa hali ya juu sana katika operesheni ambayo inaendelea hivi sasa.

Mheshimiwa Spika, nilikuwa naomba niyaseme hayo vizuri na ninarejea kwamba tumefundishwa na wazee wetu kwamba sisi kati ya mwaka 1918 na mwaka 1924 hatukuwa sehemu ya Tanganyika iliyokuwa inatawaliwa na Mwingereza. Ninaomba nirejee sisi ni watu wa Kigoma kwanza kabla hatujawa wa Tanganyika, kabla hatujawa Watanzania. Ninaomba nilisisitize hili na watu wa Kigoma wananisikia kwa sababu tumenyanyaswa sana. Ninaomba masuala ya uraia yaangaliwe kwa karibu sana. Huu ni ujumbe ambao nimepewa na watu wa Kigoma nimeombwa niueleze na naomba Ofisi ya Waziri Mkuu, Mkuu wa Kigoma yupo hapa, Wakuu wa Wilaya, Kamanda Mkuu wa Mkoa wa Polisi wa Mkoa wa Kigoma na IGP waweze kuliangalia jambo hili kuweza kuhakikisha kwamba tunawalinda raia wa Kigoma.
Wenye Mabilioni Uswisi(Switzerland)
Mheshimiwa Mwenyekiti, la pili, Mheshimiwa Waziri Mkuu kumekuwa na taarifa ambazo zimeandikwa katika vyombo vya habari toka wiki iliyopita. Lilianza Gazeti la The East AfricanThe Citizen na leo nimesikia kwamba Gazeti la Mwananchi limezungumza kwamba kuna Watanzania 6 wana fedha katika akaunti kule Uswisi zaidi ya shilingi bilioni 303. India walipopata taarifa hizi kutoka Benki ya Uswisi waliwataja majina watu wote wana siasa na wafanyabiashara wenye fedha nje na fedh zile zikachunguzwa zile ambazo zimepatikana kwa haramu zikarejeshwa India. Nilikuwa naomba Mheshimiwa Waziri Mkuu uagize TAKUKURU na vyombo vyote vya Ulinzi na Usalama kwanza tutambue ni Watanzania gani hawa na fedha hizi zimepatikana kwa njia zipi na zile ambazo zimepatikana kwa njia ya wizi na ufisadi zirejeshwe nchini mara moja. Kwa sababu hatujaanza kunyonya utajiri huu wa gesi tayari kuna watu ambao wameshaanza kutajirika nao. baadaye wakaja Gazeti la

Tutakapoanza kunyonya hali itakuwaje? Kwa hiyo, nilikuwa naomba suala hili Serikali ilichukulie kwa uzito mkubwa ili itume salaam kwa mtu yeyote ambaye anatarajia kwamba atafaidika na utajiri wa rasilimali ya nchi kama gesi na madini na kadhalika ajue kwamba kokote atakapoficha fedha zake tutazifuata na zitarudi katika nchi hii. Nilikuwa naomba Waziri Mkuu aweze kuliangalia jambo hili kwa ukaribu sana.
Zuia Makampuni ya Kigeni kwenye Ulinzi
Mheshimiwa Mwenyekiti, la tatu hivi sasa Kiongozi wa Upinzania amezungumza jana kuna meli ziko Pwani ya Mkoa wa Pwani, Lindi na Mtwara zinatafuta mafuta. Mheshimiwa Waziri Mkuu hakuna kampuni hata moja ya mafuta inayonunua hata mchicha kutoka Tanzania. Meli zote ambazo ziko Bandari Mtwara zinakwenda kupeleka huduma kwenye maeneo ambayo yanatafuta mafuta yanapata mchele, nyanya, vitunguu, mchicha, mafuta ya kula na kadhalika kutokea Kenya kwa sababu hatujaweka utaratibu wa kufanya nchi yetu iweze kufaidika na utaraji huu mwanzoni. Kwa sababu hatua hizi za mwanzoni hakuna kodi ambayo tunapata kwa sababu mafuta bado yanatafutwa.
Hatua hizi za mwanzoni tunatakiwa tufaidike na fedha inayokuja, watu waweze kutumia fedha za kutoka ndani. Lakini hali ilivyo hivi sasa ni kwamba makampuni ya mafuta yanatumia zaidi ya dola milioni 161 kwa ajili ya shughuli za ulinzi na makampuni yanayolinda, ni makampuni ya nje. Yanabeba silaha kubwa kubwa, siku yakiamua kutugeuka na Navy yetu ilivyo tutapata shida. Nilikuwa naomba tutenge resources za kutosha na hata kama hatujaziweka kwenye bajeti sasa hivi, tuangalie, tuimarishe Navy na tupige marufuku, tuandike sheria kabisa kwamba itakuwa ni marufuku kwa raia yeyote wa kigeni kubeba silaha zozote kubwa ili kuweza kuhakikisha kwamba ulinzi ama unafanywa na watu wa ndani au unafanywa na Navy yetu tuweze kulinda mipaka yetu vizuri.
Utafutaji Mafuta Zanzibar Uendelee
Mheshimiwa Mwenyekiti, pili kuna suala ambalo halijaisha na Kiongozi wa Upinzani Bungeni jana amelizungumzia la mafuta na gesi katika masuala ya muungano. Nilikuwa naomba jambo hili tulimalize kwa haraka. tulimalize kwa haraka na mimi sioni ubaya kwa kweli, sioni ubaya hata kidogo kama tukiamua kwamba shughuli zote commercial not upstream, sio masuala ya regulation, sio masuala ya vibali, sio masuala ya kutoa leseni, masuala yote commercial yanayohusiana na mafuta na gesi, kila upande wa muungano ushughulike na masuala yake.
Hakuna sababu ya kunga’gania jambo hili kama sisi tuna dhahabu, tuna tanzanite, tuna madini hayapo sehemu ya muungano, kwa nini mafuta na gesi yawe sehemu ya muungano? Hili ni jambo ambalo tulimalize, liishe tuimalize hii kero, vikao na vikao havitasaidia, tuimalize hii kero, tu-move forward watu wa Zanzibar waanze utaratibu wao wa kufanya utafutaji wao, waangalie kama watayapata hayo mafuta au hawatayapata, sisi tayari huku Bara tumeshapata, tuna matrilioni ya gesi, basin a wenyewe tuwaache waendelee na utaratibu wao. Hakuna sababu ya kuchelewesha jambo hili tuweze kulimaliza mapema.
TZS 40 Bilioni kwa Kiwira
Mheshimiwa Mwenyekiti, la mwisho ni suala la Kiwira na baadae nitakuwa na mazungumzo na baadhi ya Mawaziri kuhusiana na suala hili tuliangalie kwa makini. Tumetenga shilingi bilioni 40 kwenye fedha ya maendeleo Wizara ya Nishati na Madini kwa ajili ya nini? Kuna fedha ambayo tunaenda kuwalipa watu ambao wameuharibu mgodi. Kwa nini tulipe watu ambao wameuharibu mgodi?
Lakini tunaenda kulipa bilioni 40 sio kwa Kiwira nzima..
Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante.

kwa msaada wa; zitto kabwe.wordpress.

No comments: