Karibu kwenye Blog ya Kijamii ya Kigoma yetu kwa habari na matangazo kwa bei nafuu sana. Tunakalibisha maoni, ushauri na habari zako ili tuijenge Tanzania kwa pamoja.

Thursday, June 7, 2012

Wajasiriamali wapewa vifaa vya biashara Kigoma

SHIRIKA la Kuhudumia Viwanda Vidogo (Sido) kwa kushirikiana na Shirika la Tools for Self Reliance (TFSR) la Uingereza, wametoa vifaa vya ufundi kwa wajasiriamali wadogo mjini Kigoma kuwawezesha kukuza na kuboresha shughuli za biashara.

Meneja wa Sido mkoani Kigoma, Gervas Ntahamba alisema kuwa biashara za wajasiriamali wadogo mkoani humo zimekuwa zikizorota kutokana na mitaji midogo na uzalishaji usiozingatia viwango vya ubora, kutokana na matumizi ya vifaa duni vya kuzalishia bidhaa zao.

Akizungumza wakati wa makabidhiano ya vifaa hivyo alisema kuwa msaada huo unatokana na uhusiano mzuri kati ya Sido na shirika hilo la Uingereza kwa lengo la kuwakwamua wajasiriamali wadogo.

Ntahamba alisema wajasiriamali wamepewa mafunzo ya mbinu za kibiashara na utafutaji masoko ya bidhaa wanazozalisha. Vifaa vilivyotolewa ni vyerehani, vifaa vya ufundi seremala na uhunzi.

Mkurugenzi wa Manispaa ya Kigoma Ujiji, Alfred Luanda aliwataka wajasiriamali hao kutumia vifaa hivyo kwa malengo yaliyokusudiwa ili vilete tija na kuwakwamua kutoka hatua waliyopo.

No comments: