Karibu kwenye Blog ya Kijamii ya Kigoma yetu kwa habari na matangazo kwa bei nafuu sana. Tunakalibisha maoni, ushauri na habari zako ili tuijenge Tanzania kwa pamoja.

Tuesday, June 12, 2012

Anna Wilbroad ndiye Miss Kigoma


Miss Kigoma 2012 Anna Willboad (aliyeketi) akiwa na Mshindi wa pili ni Suzan Gregory (wa pili kulia) na mshindi wa watu, Justina Philipo baada ya kutwaa taji hilo juzi.Kulia ni Mkurungenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kigoma, Lilian Mbaga.

MWANADADA Anna Wilbroad juzi usiku alifanikiwa kunyakua taji la mnyange wa Kigoma kwa mwaka 2012 baada ya kuwashinda washiriki wenzake saba walioshiriki kinyang’anyiro hicho.

Akitangaza matokeo ya ushindi, jaji mkuu wa mashindano hayo Rashidi Michumino kutoka ofisi ya mkurugenzi wa manispaa ya Kigoma Ujiji, alisema kuwa pamoja na kunyakua taji hilo mnyange huyo pia amepata zawadi ya fedha Sh 300,000 na kushiriki katika mashindano ya kanda mkoani Dodoma.

Pamoja na zawadi hizo pia mshindi huyo amepata zawadi ya kusoma kozi ya masomo ya utalii kwa mwaka mmoja katika chuo cha Western Tanganyika cha mjini Kigoma.

Mshindi wa pili katika shindano hilo alikuwa mrembo Susan Gregory aliyepata zawadi ya Sh 200,000, kozi ya masomo ya utalii kwa mwaka mmoja akipata nafasi pia ya kushiriki mashindano ya ngazi ya kanda mkoani Dodoma.

Jaji wa shindano alimtangaza mwanadada Justina Philipo kuwa mshindi wa tatu ambaye alipata zawadi ya fedha taslim Sh 100,000, kozi ya computer, pia akapata nafasi ya kushiriki katika mashindano ngazi ya Kanda.

Mwanadada Mwamvita Juma aliibuka kuwa mshindi katika shindano la vipaji na ubunifu ambapo alizawadiwa Sh 50,000 katika shindano ambalo Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya Kigoma, Lilian Mbaga alikuwa mgeni rasmi.

Akikabidhi zawadi kwa washindi Mkurugenzi huyo wa Halmashauri ya wilaya 
Kigoma alitoa wito kwa wazazi kuwaruhusu
watoto wao kushiriki shindano hilo ambalo kwa sasa limekuwa pia chanzo cha ajira 
kwa wasichana wanaofanya vizuri na wenye vipaji.


No comments: