Karibu kwenye Blog ya Kijamii ya Kigoma yetu kwa habari na matangazo kwa bei nafuu sana. Tunakalibisha maoni, ushauri na habari zako ili tuijenge Tanzania kwa pamoja.

Tuesday, June 26, 2012

Abaka akidai anafanya tambiko Kigoma



POLISI mkoani Kigoma imemtia mbaroni mfanyabiashara wa mjini Kigoma, Nuru Juma maarufu Baba Kadindile kwa tuhuma za kumbaka msichana mwenye miaka 16 baada ya kumlaghai kuwa anamfanyia tambiko.

Kamanda wa Polisi Mkoa, Fraisser Kashai aliwambia waandishi wa habari mjini hapa kwamba Baba Kadindile mkazi wa Mwandiga anatuhumiwa kumbaka msichana huyo mwishoni mwa wiki iliyopita saa nne usiku ambapo alimlaghai msichana huyo aingie chumbani kwake ili amfanyie tambiko.

Baba Kadindile ambaye alipata umaarufu kwa kupata fedha kutoka maeneo mbalimbali ya nyumba yake alizokuwa akizipata kwa kuoteshwa na mizimu, alizidi kujijengea umaarufu huo kwa kununua magari na vitu mbalimbali kwa fedha taslimu ambapo fedha hizo zikiwa haziwekwi benki.

Kamanda Kashai alisema kuwa baada ya kumtia mbaroni mtuhumiwa huyo, upelelezi kuhusu tuhuma hizo unaendelea ili kumfikisha mtuhumiwa mahakamani kujibu tuhuma zinazomkabili
Katika tukio lingine Kamanda huyo wa Polisi alisema bunduki nane za SMG na risasi 232 zimekamatwa katika maeneo mbalimbali ya Mkoa Kigoma katika operesheni maalumu iliyofanywa na askari Polisi kwa kushirikiana na vikosi vingine vya ulinzi na usalama katika kipindi cha wiki mbili zilizopita.

Aidha Polisi wamekamata pia magobore mawili na watu wawili inawashikilia kwa kuhusika na baadhi ya silaha zilizokamatwa

No comments: