Karibu kwenye Blog ya Kijamii ya Kigoma yetu kwa habari na matangazo kwa bei nafuu sana. Tunakalibisha maoni, ushauri na habari zako ili tuijenge Tanzania kwa pamoja.

Friday, June 22, 2012

David Kafulila dai Bunge linanuka rushwa



Mbunge wa Kigoma Kusini, David Kafulila (NCCR Mageuzi)


MBUNGE wa Nkasi Kaskazini, Mohamed Keisy (CCM) amesema wabunge pamoja na taasisi ya Bunge vinanuka rushwa na kutaka Chama cha Wabunge Wanaopambana na Rushwa (APNAC), kuchukua hatua za haraka kurekebisha suala hilo.

Akizungumza jana katika semina ya wabunge ambao ni wanachama wa APNAC, Keisy alisema kitendo cha wabunge kunuka rushwa sio kizuri hata kidogo kwani watakosa nguvu za kukemea suala hilo.
“Mwenyekiti wabunge wananuka rushwa na Bunge limegubikwa na fununu za rushwa ambazo ni nyingi, hivi tufanyeje kwenye suala hili? alihoji mbunge huyo.

Wabunge ambao ni wanachama wa APNAC waliandaliwa semina hiyo na asasi isiyo ya kiserikali ya Policy Forum kwa ajili ya kuzindua ripoti kuhusu ushindani wa kodi ndani ya Afrika Mashariki hususani upotevu wa mapato nchini katika masuala ya kodi.

Mbunge huyo pia katika mchango wake, alitaka watu wajitume kufanya kazi badala ya kuilaumu Serikali kuwa maisha ni magumu wakati wananchi wengi hasa wa mwambao wa Pwani hawataki kufanya kazi.

Wakati huo huo, Mbunge wa Kigoma Kusini, David Kafulila (NCCR Mageuzi) ameliambia gazeti hili jana kuwa ameshaandika barua ya kujiuzulu ujumbe wa Kamati ya Bunge ya Serikali za Mitaa (LAAC) kutokana na kamati hiyo kunuka rushwa.

Kafulila alisema ameandika barua hiyo Ijumaa wiki iliyopita na kuiwasilisha kwa Spika wakiwa bado jijini Dar es Salaam kutimiza azma yake ya kujiondoa kwenye kamati hiyo ambayo alisema haina maadili hata kidogo.

“Mle ndani ya kamati wala rushwa ni wengi, suala ni kuzidiana tu na hata siku ya tukio ambayo mmoja wetu alikamatwa, kuna mjumbe mwingine (jina tunalo) alichelewa tu kwenye foleni naye alikuwa ameahidiwa kwenda kuchukua fedha hizo,” alidai Kafulila.

No comments: