Karibu kwenye Blog ya Kijamii ya Kigoma yetu kwa habari na matangazo kwa bei nafuu sana. Tunakalibisha maoni, ushauri na habari zako ili tuijenge Tanzania kwa pamoja.

Wednesday, May 30, 2012

Kigoma waikumbuka Mbanga FC

CHAMA cha soka mkoani Kigoma (KRFA) kimesema kuwa kushuka kwa timu za soka za Mbanga na Congo Fc zilizokuwa zikishiriki Ligi Kuu Tanzania Bara, kumechangia kushusha morali ya wapenzi wa soka mkoani hapa na kususa kujitokeza uwanjani sambamba na kukataa
kuchangia fedha kusaidia timu za mkoa huo zinazoshiriki kwenye michuano mbalimbali ndani na nje ya mkoa.

Akizungumza mjini hapa juzi, Katibu wa chama hicho Mrisho Bukuku alisema, tangu kuanza kwa mashindano ya ligi ta taifa ngazi ya taifa kituo cha Kigoma kumekuwa na watazamaji kidogo wanaojitokea uwanjani kushuhudia mechi mbalimbali.

Alisema, hali hiyo imechangia timu za mkoa huo kufanya vibaya kwenye michuano mbalimbali kutokana na maandalizi duni yanayosababishwa na ukosefu wa fedha za maandalizi ya timu.

Akitoa mfano alisema, hata kwenye michuano ya Copa Coca- Cola ambayo mkoa huo imekuwa ikishiriki na kufanya vizuri kwa kiasi kikubwa, ufadhili wa kuwezesha timu ya mkoa huo kushiriki michuano hiyo umekuwa ukitoka kwa wahisani nje ya mkoa huo.

Aidha alisema, hivi sasa mkakati wa uongozi wa soka mkoani hapa kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wakiongozwa na Mkurugenzi wa manispaa ya Kigoma Ujiji, John Luanda ni kuhakikisha timu ya JKT Kanembwa ambayo kwa sasa inashiriki ligi kuu ya taifa ngazi ya
taifa kituo cha Kigoma inafanya vizuri na kupata nafasi ya kushiriki Ligi Kuu.

Wakati Bukuku akieleza hilo baadhi ya wapenzi wa soka mkoani hapa wamelalamikia viongozi wa KRFA na chama cha soka manispaa ya Kigoma Ujiji (KUFA) vimechangia kufanya vibaya kwa timu za mkoa huo na kushusha morali ya wananchi kupenda na kuchangia michezo.

Wastara Baribari mchezaji wa zamani wa timu ya RTC Kigoma na Pamba ya Mwanza alisema kuwa uongozi wa soka wa mkoa na wilaya unapaswa kubeba lawama zote za kushuka kwa kiwango cha soka mkoani humo kwani viongozi hao hawana mkakati wowote wa kuendeleza
michezo zaidi ya kuangalia maslahi yao ya namna gani watapata pesa kupitia vyama hivyo.

 

No comments: