Karibu kwenye Blog ya Kijamii ya Kigoma yetu kwa habari na matangazo kwa bei nafuu sana. Tunakalibisha maoni, ushauri na habari zako ili tuijenge Tanzania kwa pamoja.

Friday, April 27, 2012

Balozi ahimiza jamii kusaidia yatima - Kigoma

 Balozi wa Marekani nchini,Alfonso Lenhardt

BALOZI wa Marekani nchini,Alfonso Lenhardt ametaka jamii iwasaidie wanafunzi yatima ambao walezi wao hawana uwezo wa kuwapatia elimu ya kutosha na kutimiza ndoto zao.

Lenhardt alisema hayo mjini Kigoma juzi alipotembelea Taasisi ya Western Tanganyika Trust inayojishughulisha kuwasomesha watoto yatima.


Balozi Lenhardt alisema yatima na wanaoishi kwenye mazingira magumu wanayo nafasi na

mchango mkubwa wa kuleta maendeleo kwa jamii zao na nchi kwa jumla kama wataendelezwa
na kupewa nafasi.

Zaidi katika hotuba yake hiyo, Balozi huyo wa Marekani ametaka kipaumbele kitolewe kwa watoto wa kike na hasa kutokana na hali zao na changamoto zinazowakabili katika kupata elimu.


Katika ziara hiyo, Balozi Lenhardt amevutiwa na mpango wa Taasisi ya Western Tanganyika

Trust katika kuendesha mpango wa kusomesha watoto yatima na wsiojiweza na kuuelezea kwamba ni mpango ambao unalenga katika ukombozi wa baadaye wa watoto wao.

Awali, Mratibu Miradi wa WTT, Richard Makulilo alimwambia Balozi huyo kwamba watoto 131 wanasomeshwa na taasisi hiyo kwa ngazi mbalimbali za elimu ikiwamo msingi, sekondari na vyuo.

No comments: