Karibu kwenye Blog ya Kijamii ya Kigoma yetu kwa habari na matangazo kwa bei nafuu sana. Tunakalibisha maoni, ushauri na habari zako ili tuijenge Tanzania kwa pamoja.

Saturday, March 3, 2012

Tume yaundwa Kigoma kuchunguza askari ‘wahalifu’

POLISI mkoani Kigoma imeunda Tume ya kufanya uchunguzi wa tuhuma zinazowakabili baadhi ya askari mkoani humo kuhusu usafirishaji haramu wa pembe za ndovu kwenda nchini jirani ya Burundi.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa, Fraiser Kashai alisema jana kuwa tume hiyo ya uchunguzi itaongozwa na Mkuu wa Upelelezi wa Mkoa, Joseph Konyo kwa nia ni kufanya uchunguzi wa kina kujua undani wa jambo hilo.


Kashai alisema kuundwa kwa Tume hiyo, kunatokana na habari zilizoandikwa na gazeti moja la kila siku kuhusu kuwepo kwa askari Polisi waliokuwa wakihusika na usafirishaji huo wa pembe za ndovu kwenda nchi za jirani.


Alisema mbali na kuongozwa na Mkuu wa Upelelezi wa Mkoa, pia Tume hiyo itawajumuisha maofisa wengine kutoka Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), Idara ya Uhamiaji, Usalama wa Taifa na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru).


Katika tukio lingine, mwanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Kagongo Kigoma Vijijini, amekufa wakati akiogelea eneo la Kibirizi kando ya Ziwa Tanganyika mjini Kigoma.


Kamanda Kashai amemtaja mtoto huyo kuwa Saidi Juma na alikufa juzi saa 2 usiku katika eneo hilo na mwili wake ulipatikana na kukabidhi kwa ndugu zake kwa ajili ya mazishi baada ya kufanyiwa uchunguzi.

No comments: