Karibu kwenye Blog ya Kijamii ya Kigoma yetu kwa habari na matangazo kwa bei nafuu sana. Tunakalibisha maoni, ushauri na habari zako ili tuijenge Tanzania kwa pamoja.

Wednesday, March 28, 2012

Kutoelewa sheria sababu ya uharibifu wa mazingira

VIONGOZI wa vijiji na wa kamati za mazingira wamedaiwa kutofahamu sera na sheria za utunzaji kiasi cha kusababisha uharibifu wa mazingira vijijini.

Mhadhiri wa chuo kikuu cha kilimo cha Sokoine (SUA), Profesa Alexanda Songorwa amesema hayo katika mahojiano maalumu wakati wa mafunzo ya siku 10 kwa wajumbe wa kamati za mazingira za vijiji kutoka halmashauri ya wilaya Kigoma.


Alisema kwa sasa uharibifu mkubwa wa mazingira umehamia vijijini kutokana na harakati nyingi za maendeleo kuhamia kwenye utafutaji wa maeneo ya uwekezaji.


Mtaalamu huyo wa mazingira alibainisha kuwa uharibifu mkubwa wa mazingira unachangiwa na matumizi yasiyozingatia sheria za mazingira na hasa kasi kubwa ya utwaaji maeneo hayo.


Alisema wawekezaji Wengi hawaoni manufaa kiuchumi wanapofika vijijini kwa ajili ya kutwaa

maeneo.

Alisema kuwa katika kuonesha kuwa sera na sheria za mazingira kwao ni tatizo baadhi ya kamati za mazingira za vijiji zimekuwa zikigeuzwa kuwa kamati za matumizi bora ya ardhi na hivyo wakati mwingine kufanya kazi tofauti badala ya kusimamia utunzaji na ulinzi wa mazingira katika maeneo yao.


Kassim Sengo mmoja wa washiriki hao alisema kuwa kamati za mazingira katika baadhi ya vijiji ambako wamepata ushirikiano mzuri na serikali za vijiji zimefanya kazi nzuri katika utunzaji mazingira na uhifadhi ikiwemo utengaji wa baadhi ya maeneo kwa ajili ya kuhifadhi msitu.


Mratibu wa mafunzo hayo Valentine Kabadi ambaye ni ofisa uvuvi wa halmashauri ya wilaya Kigoma alisema kuwa jumla ya washiriki 25 kutoka maeneo mbalimbali ya halmashauri hiyo wamehudhuria mafunzo ambayo lengo ni kuwakumbusha sheria na sera za utunzaji mazingira.

No comments: