Karibu kwenye Blog ya Kijamii ya Kigoma yetu kwa habari na matangazo kwa bei nafuu sana. Tunakalibisha maoni, ushauri na habari zako ili tuijenge Tanzania kwa pamoja.

Wednesday, March 28, 2012

Jaji akataa kujitoa kesi ya Serukamba

OMBI la mlalamikaji katika kesi ya kupinga matokeo ya ubunge wa Jimbo la Kigoma lililompa ushindi mbunge wa jimbo hilo Peter Serukamba, la kutaka Jaji wa kesi hiyo Stella Mugasha kujitoa limegonga mwamba.

Akitoa uamuzi kuhusu ombi hilo, Jaji Mugasha alisema kuwa kwa mujibu wa kifungu cha 2(c) 1 cha Mwongozo wa Maadili wa Maofisa wa Mahakama nchini ombi la mlalamikaji katika shauri

hilo halikuzingatia vionjo vya mwongozo huo.

Alisema kuwa binafsi hana maslahi ya namna yoyote katika shauri hilo na kwa maana hiyo

hatajitoa na kutoa uamuzi kwamba baada ya kauli yake hiyo mahakama inaendelea na shauri
hilo.

Hata hivyo, baada ya kauli hiyo ya Jaji Mugasha, Mawakili wa upande wa mlalamikaji katika kesi hiyo, Anney Semu na Emmanuel Kessy ambao waliwasilisha ombi la mteja wao la kutokuwa na imani na jaji anayesikiliza kesi hiyo walitangaza kujitoa kuendelea na kesi hiyo.


Awali wakili Semu akisoma barua iliyowasilishwa mahakamani hapo asubuhi jana kabla ya

kuanza kwa kesi hiyo alisema kuwa mteja wake hana imani na Jaji Mugasha kutokana na vipengele vitatu ambavyo alivitaja kuwa ni pamoja na kitendo cha jaji huyo kukataa kupokea kanda za video kama moja ya vielelezo vya ushahidi.

Hoja hizo za upande wa mlalamikaji zilipingwa na wakili Kennedy Fungamtama anayemtetea mlalamikiwa wa kwanza Peter Serukamba na mlalamikiwa wa tatu msimamizi wa uchaguzi wa jimbo la Kigoma mjini.


Katika kupinga hoja hiyo, Wakili Fungamtama alitoa mifano ya kesi tatu ikiwemo kesi ya

Yussuf Manji na Quality Group dhidi ya Mchungaji Christopher Mtikila ambapo upande mmoja
ulimkataa jaji wa kesi hiyo, Jaji Mihayo na uamuzi uliposikilizwa shauri hilo lilitupwa.

Akisisitiza kutupwa kwa shauri hilo la kumkataa jaji wa kesi hiyo, Wakili Fungamtama alisema kuwa ili jaji aweze kujitoa anapaswa kuwa na uhusiano wa karibu na upande mmoja wa kesi

hiyo, kuwa na maslahi binafsi na kesi hiyo au kwenda kinyume na sheria, kanuni na miongozo ya utendaji haki kitu ambacho kwa kesi hiyo hakipo.

Jaji Mugasha alitoa siku nne mlalamikaji katika kesi hiyo awe amepata mawakili wapya hadi

kufikia Machi 27 na kwamba shauri hilo litaendelea tena mahakamani Machi 28 mwaka huu.

No comments: