Karibu kwenye Blog ya Kijamii ya Kigoma yetu kwa habari na matangazo kwa bei nafuu sana. Tunakalibisha maoni, ushauri na habari zako ili tuijenge Tanzania kwa pamoja.

Saturday, February 25, 2012

Mv Liemba Kigoma kufanyiwa matengenezo makubwa




MKUU wa Mkoa wa Rukwa, Mhandisi Stella Manyanya amebainisha kuwa Bandari ya Kasanga iliyopo katika mwambao wa Ziwa Tanganyika wilayani Sumbawanga inahudumiwa na meli ya
mv Liemba inayosadikiwa kuwa meli yenye umri mkubwa duniani.

Meli hiyo mbali ya kuhudumia Bandari za Kigoma na Kasanga lakini pia inatoa huduma katika
nchi jirani za Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Zambia, Rwanda na Burundi.

Akisoma taarifa ya maendeleo ya mkoa mbele ya Makamu wa Rais, Dk. Mohamed Gharib Bilal, Manyanya alisema kutokana na kuzeeka kwa meli hiyo iliyotengenezwa nchini Ujerumani karne moja iliyopita inatazamiwa kufanyiwa matengenezo makubwa kwa fedha
zitakazotolewa na nchi hiyo ya Ujerumani.

Makamu wa Rais alielezwa kuwa meli hiyo ilikaa muda mrefu bila kufanya kazi hadi mwaka 1996 ilipoanza usafirishaji wa abiria katika Bandari ya Kasanga ambayo ni ya pili baada ya Bandari ya Kigoma ambapo ilianza pia kubeba mizigo mwaka 2003.

“Meli hii ya mv Liemba kwa sasa inabeba pia mizigo kutoka bandari ya Kasanga na kuisafirisha
mizigo hiyo ikiwemo saruji kwenda bandari ya Kigoma na nchi jirani za DRC, Rwanda, Zambia na Burundi.

Na kufikia Desemba 2011 meli hiyo ilikuwa tayari imesafirisha tani 117,823.86 za mizigo, “ alisema Manyanya.

Alizitaja changamoto kadhaa zinazoikabili Bandari hiyo ya Kasanga kuwa ni pamoja na ukosefu wa huduma ya umeme wa uhakika, safari chache zinazofanywa kwa mwezi na miundombinu ya barabara kutoka Sumbawanga kwenda Kasanga kuwa mibovu.

No comments: