BENKI ya Posta Tanzania imesema ipo katika mkakati wa kuboresha maeneo
yake ya utoaji huduma sambamba na kuboresha huduma zake na kuvutia
wateja.
Mkurugenzi Mtendaji wa benki hiyo, Sabasaba Moshingi alisema hayo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari wakati wa hafla ya kukabidhi misaada mbalimbali yenye thamani ya Sh milioni 1.2 iliyotolewa na benki hiyo kwa nyumba ya wazee wasiojiweza Kibirizi mjini Kigoma.
Alisema kuwa miongoni mwa maboresho hayo ni pamoja na kufungua matawi katika majengo yanayovutia yenye hadhi ya kibenki sawa na benki nyingine nchini.
Aidha alisema kuwa mkakati mwingine ni kuongeza wateja ambao wamekuwa na msongamano mkubwa katika kupata huduma kwenye benki nyingine.
Kwa upande wake Meneja wa Benki ya Posta Mkoa Kigoma, Juma Kanyeti ameitaja misaada iliyotolewa na benki hiyo kuwa ni pamoja na mahindi kilo 800, maharage kilo 400, mafuta ya kupikia lita 60 na sabuni za kuogea na kufulia katoni tano.

No comments:
Post a Comment