Karibu kwenye Blog ya Kijamii ya Kigoma yetu kwa habari na matangazo kwa bei nafuu sana. Tunakalibisha maoni, ushauri na habari zako ili tuijenge Tanzania kwa pamoja.

Saturday, February 25, 2012

Huduma ya Ultra Sound yakosekana Kigoma

HOSPITALI ya Mkoa wa Kigoma ya Maweni haina huduma ya vipimo vya Ultra Sound kwa kipindi cha miezi mitatu sasa, hali ambayo imeleta usumbufu kwa wakazi zaidi ya 250,000 wa Manispaa ya Kigoma Ujiji wanaotegemea huduma hiyo kutoka hospitalini hapo.

Wakizungumza na waandishi wa habari jana katika Hospitali ya Mkoa ambapo walikuwa wakitarajia kupata huduma hiyo, wananchi hao walisema kuwa wanalazimika kulipa gharama kubwa katika hospitali binafsi mara mbili ya ile waliyokuwa wakilipa Hospitali ya Mkoa.


Mmoja wa wananchi hao Mariam Kassim mkazi wa Ujiji mjini Kigoma alisema kuwa kwa sasa wanalazimika kulipa hadi Sh 12,000 katika hospitali binafsi badala ya Sh 5,000 waliyokuwa wakilipa Hospitali ya Mkoa kwa ajili ya huduma hiyo.


Mganga Mfawidhi wa Hospitali hiyo ya Mkoa Kigoma ya Maweni, Dk. Macrice Yakayashi alikiri kutokuwepo kwa huduma hiyo ya ultra sound kwa muda mrefu sasa na kwamba uongozi wa hospitali umejipanga kuhakikisha huduma hiyo inarudishwa katika kipindi kifupi kijacho.


Dk. Yakayashi alisema kuwa kinachokwamisha kurudishwa kwa huduma hiyo kwa haraka ni taratibu za sheria ya manunuzi ya Serikali ambayo mzunguko wake unachangia kufanya manunuzi hayo kuchukua muda mrefu.


Pamoja na hilo alisema kuwa hospitali hiyo iko kwenye mkakati wa kufanya manunuzi ya vifaa mbalimbali vya upimaji vya kisasa ikiwa ni mkakati wa uboreshaji huduma katika Sekta ya Afya.

No comments: