Karibu kwenye Blog ya Kijamii ya Kigoma yetu kwa habari na matangazo kwa bei nafuu sana. Tunakalibisha maoni, ushauri na habari zako ili tuijenge Tanzania kwa pamoja.

Thursday, January 5, 2012

Leseni zatibua mipango ya safari

ZAIDI ya abiria 350 waliokuwa wakisafiri kwa mabasi ya kampuni mbalimbali kwenda nje ya Mkoa Kigoma wamekwama mjini hapa kwa zaidi ya saa sita baada ya polisi wa Usalama barabarani kuwazuia madereva wa magari hayo kutokana na kutokuwa na leseni mpya.

Mwandishi wa habari hizi alishuhudia juzi mamia ya abiria hao wakiwa katika kituo cha mabasi
wengi wao wakilalamikia kitendo hicho kwamba kimewaharibia ratiba zao za safari na shughuli zao.

Mabasi yaliyozuiliwa ni pamoja na lile la Kampuni ya Golden Inter State linalokwenda Mwanza, Sasebosa la kwenda Tabora, Ally’s Sports la Kahama na YAAlY la kwenda Bukoba.

Wakizungumza na waandishi wa habari kituoni hapo baadhi ya madereva wa mabasi yaliyozuiliwa wamelalamikia kitendo hicho.

Ally Salum dereva wa Kampuni ya Sasebosa ya mjini Tabora alisema kuwa polisi walipaswa kutoa taarifa kuweka siku ya mwisho kwao lakini pia wakipewa kipaumbele katika kushughulikia jambo hilo.

Alisema kuwa chuo kilikuwa kinaendesha mafunzo lakini baadaye chuo hicho kikasimamisha
madereva wakatakiwa kutafuta chuo kingine lakini pia mfumo wa kompyuta katika Mamlaka ya Mapato (TRA) umekuwa ukisumbua.

Wameishauri kutokana na hilo wameitaka serikali kuangali upya mkakati wao wa kuwazuia madereva wasio na leseni mpya kufanya safari na kwamba kuanzia sasa wanapaswa wawape muda kushughulikia jambo hilo.

Kamanda wa Polisi Mkoa Kigoma, Fraiser Kashai alikiri kuzuiwa kwa magari hayo kutokana na
madereva wake kutokuwa na leseni mpya na kusema kuwa mabasi yote yanayoenda nje ya mkoa yalikamatwa lakini baadhi, yalileta madereva wenye leseni na safari zao zikaendelea.

Aidha Kamanda Kashai alikiri kuwepo kwa matatizo katika mfumo mzima wa mawasiliano ya
kompyuta katika kushughulikia suala hilo.

Hata hivyo alisema hilo halizuii dereva kutotimiza masharti ya kuwa na leseni mpya. Aliendelea kusisitiza madereva wasio na leseni kutoendesha magari.

 

No comments: