MJI wa Kigoma Ujiji na vitongoji vyake hauna huduma ya maji inayotolewa na Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Kigoma Ujiji (KUWASA) kwa zaidi ya siku nne sasa kutokana na kukatiwa umeme katika mitambo yake ya kusukumia maji. Mkurugenzi Mtendaji wa Kuwasa, Saimon Lupuga amethibitisha kutokuwepo kwa huduma hiyo tangu mwanzoni mwa wiki hii na kusema kuwa hali hiyo inatokana na kukatwa kwa huduma ya umeme katika mitambo yake ya kusukumia maji iliyopo Bangwe mjini Kigoma. Lupuga alisema kuwa kitendo cha mamlaka yake kukatiwa maji kwa siku ya nne kimetokana na kudaiwa na Shirika la Umeme (TANESCO) Mkoa Kigoma kiasi cha Sh milioni 321 ikiwa ni madai ya matumizi ya umeme iliokuwa ukitolewa kwenye mitambo hiyo ya kusukumia maji. Mkurugenzi huyo amekiri kuwepo kwa deni la muda mrefu ambalo Tanesco inaidai Kuwasa na kwamba deni hilo lilirithiwa na mamlaka hiyo kutoka iliyokuwa Idara ya Maji. Mbali na kuendelea kwa deni hilo, pia Mkurugenzi huyo alikiri kuwa deni limeongezeka kutokana na makusanyo yanayofanywa na mamlaka hiyo kutokidhi ulipaji wa matumizi ya umeme wanayotumia kwa mwezi. Akizungumzia hali hiyo, Meneja wa Tanesco Mkoa wa Kigoma, Cleophasi Tibaijuka alisema kuwa shirika hilo linajiendesha kibiashara na limekuwa likigawia Kuwasa umeme wenye thamani kati ya Sh milioni 43 na 44 kila mwezi. Tibaijuka alisema kuwa wamekuwa wakitoa kipaumbele kwa mitambo ya kusukuma maji ya Kuwasa kutokana na unyeti wa huduma hiyo kwa jamii lakini ulipaji wa deni hilo kutokana na matumizi ya umeme wanaotumia umekuwa wa kusuasua sana. |
Kuna Ziwa Tanganyika, Makumbusho ya Livingstone Ujiji, Hifadhi za Gombe na Mahale, Migebuka, Mawese na Dagaa wakutosha.
Tuesday, January 3, 2012
Kigoma yakabiliwa na uhaba wa maji
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment