Karibu kwenye Blog ya Kijamii ya Kigoma yetu kwa habari na matangazo kwa bei nafuu sana. Tunakalibisha maoni, ushauri na habari zako ili tuijenge Tanzania kwa pamoja.

Monday, January 16, 2012

Huduma za treni Dar-Kigoma kuanza jumatano

uduma za safari za treni za abiria za Kampuni ya Reli Tanzania -TRL kutoka Dar es Salaam kwenda Kigoma zinatarajiwa kuanza keshokutwa ambapo abiria wanaweza kuanza kukata tiketi hii leo katika stesheni husika.
 
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na TRL, kuanza tena kwa huduma hiyo kumetokana na kukamilisha kazi ya ukarabati ambayo imewezesha treni za mizigo zipatazo 10 kutoka na kwenda bara kupita eneo la Godegode mkoani Dodoma.

Hata hivyo mafundi wa TRL bado wanaendelea na kazi ya kuimarisha tuta la reli katika maeneo mawili korofi eneo la Stesheni ya Godegode ambayo hukumbwa na mafuriko na kusababisha reli kuharibika.

Huduma  za treni zilisimamishwa Januari 07, 2012  baada ya kutokea uharibifu mkubwa katika eneo la stesheni ya Godegode kufuatia mafuriko yaliyokumba eneo hilo baada ya mvua kubwa kunyesha katika mikoa ya Morogoro, Iringa na Dodoma.

No comments: