Karibu kwenye Blog ya Kijamii ya Kigoma yetu kwa habari na matangazo kwa bei nafuu sana. Tunakalibisha maoni, ushauri na habari zako ili tuijenge Tanzania kwa pamoja.

Sunday, December 4, 2011

RC akerwa na harufu ya uchafu Kigoma

MKUU wa Mkoa wa Kigoma, Issa Machibya amewataka viongozi na wananchi katika Manispaa ya Kigoma kufanya jitihada katika kutekeleza mradi wa kuusafisha mji huo ili hali iliyo sasa ya mji huo kunuka kwa uchafu iwe historia.

Machibya aliyasema hayo wakati akifungua mkutano wa siku mbili ulioandaliwa na mradi wa hifadhi ya Ziwa Tanganyika uliokuwa ukishirikisha wadau zaidi ya 700 kutoka katika Manispaa ya Kigoma Ujiji ambao ulilenga kutoa elimu na uhamasishaji wa kuuweka mji huo katika hali ya usafi.


Mkuu huyo wa Mkoa alisema kuwa hali ya sasa ya manispaa kuzalisha tani 122 huku ikiwa na uwezo wa kuzoa tani 68 sawa na asilimia 56.8 ya taka zinazozalishwa ina uweka mji katika hali isiyopendeza na ambayo si salama kwa afya za wananchi na wakazi wa mji huo.


Awali, Ofisa Afya wa Manispaa ya Kigoma Ujiji, Ernest Nkonyozi alisema kuwa katika uchambuzi walioufanya matatizo sita yamebainika ambayo ni pamoja na uelewa mdogo wa wananchi juu ya usafi na utunzaji mazingira, utupaji hovyo wa taka na ukosefu wa vyoo bora.


Matatizo mengine aliyataja kuwa ni pamoja na kudhurika kwa afya za watu kutokana na magonjwa ya tumbo, kutoweka kwa viumbe hai na kupungua kwa kina cha maji katika ziwa Tanganyika.

No comments: