Karibu kwenye Blog ya Kijamii ya Kigoma yetu kwa habari na matangazo kwa bei nafuu sana. Tunakalibisha maoni, ushauri na habari zako ili tuijenge Tanzania kwa pamoja.

Sunday, November 20, 2011

Veta yafunga vyuo 48 vya ufundi stadi Kanda ya Magharibi

MAMLAKA ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi Tanzania (VETA) imevifunga vyuo 48 vya ufundi stadi katika Kanda ya Magharibi baada ya kukosa sifa ya kufundisha masomo ya elimu ya ufundi stadi kwa vijana.
Akizungumza na waandishi wa habari mjini Tabora mwishoni mwa wiki, Mkurugenzi wa VETA wa Kanda ya Magharibi, Hildegadis Bitegera, alisema vyuo hivyo vimefungwa katika eneo la kanda hiyo linalojumuisha mikoa ya Tabora, Kigoma na Shinyanga.

Bitegera alisema kufungwa kwa vyuo hivyo kumetokana na ukaguzi uliofanywa na mamlaka hiyo katika mikoa hiyo na hatua hiyo itasaidia kuondokana na tatizo la kuwepo kwa vyuo visivyokuwa na sifa hivyo kusababisha kuwepo kwa wahitimu wasiofaa.


Alisema chini ya ukaguzi huo, vyuo 28 vya Serikali na taasisi mbalimbali vimeruhusiwa kuendelea na mchakato wa utoaji wa mafunzo hayo ya elimu ya ufundi stadi katika mikoa hiyo baada ya vyuo hivyo kukidhi viwango vya utoaji wa elimu ya ufundi stadi.


Alisema mamlaka yake itaendelea na ukaguzi wa mara kwa mara utakaosaidia kuhakikisha kuwa vyuo vyote vinavyotoa elimu ya ufundi stadi katika mikoa hiyo vinatimiza wajibu wake ipasavyo na hivyo kupatikana kwa wahitimu wenye stadi na ujuzi unaotakiwa katika soko la ajira.


Mapema, Mkurugenzi huyo aliwataka waajiri wa sekta ya ufundi katika kanda hiyo kuhakikisha

kuwa wanaajiri vijana wenye uwezo wa kukidhi viwango vya mahitaji ya soko katika ngazi ya Afrika Mashariki na kimataifa ambao wanahitimu katika vyuo vinavyotambuliwa na Serikali.

No comments: