Karibu kwenye Blog ya Kijamii ya Kigoma yetu kwa habari na matangazo kwa bei nafuu sana. Tunakalibisha maoni, ushauri na habari zako ili tuijenge Tanzania kwa pamoja.

Tuesday, October 11, 2011

RC Kigoma aridhishwa kasi ya ujenzi wa barabara

Mkuu wa mkoa wa Kigoma Luteni Kanali Mstaafu Issa Machibya ameelezea kuridhishwa kwake na kasi ya ujenzi wa kiwango cha lami wa barabara ya Kidahwe hadi Uvinza yenye urefu wa Kilometa 76 pamoja na ujenzi wa daraja la mto Malagarasi lenye urefu wa mita 275.

Luteni Kanali Mstaafu Machibya ametoa kauli hiyo baada ya kutembelea maeneo mbalimbali ya utekelezaji wa miradi hiyo, ziara ambayo alifuatana na wataalam wa sekta mbalimbali, wajumbe wa kamati ya ulinzi na usalama, pamoja na wakandarasi wanaotekeleza miradi hiyo.


No comments: