Karibu kwenye Blog ya Kijamii ya Kigoma yetu kwa habari na matangazo kwa bei nafuu sana. Tunakalibisha maoni, ushauri na habari zako ili tuijenge Tanzania kwa pamoja.

Wednesday, October 12, 2011

Mustafa Mkulo,mikoa ya Kigoma, Iringa na Shinyanga kuunganisha umeme katika mikoa hiyo

SERIKALI inatarajia kuanza kuwalipa fidia ya Sh bilioni 1.48 wananchi 614 wa Mloganzila wilayani Kinondoni mkoani Dar es Salaam ambao wamefanyiwa tathmini kwa awamu ya pili. 
Akizungumza jana Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Mradi wa Ujenzi wa Chuo Kikuu cha Sayansi ya Tiba na Afya Muhimbili (MUHAS) kinachojengwa katika eneo hilo, Dk. Appolinary Kamuhabwa alisema ulipaji huo unatarajiwa kuanza hivi karibuni.

Dk. Kamuhabwa alisema katika awamu ya kwanza, wananchi 1,919 wamelipwa Sh bilioni 8.06 kwa ajili ya fidia ya mali na mazao na kwa upande wa ardhi unaangaliwa na Serikali.

Alisema hayo katika hafla ya kusaini mkataba wa Dola za Marekani milioni 63.4 sawa na Sh bilioni 103.6, kati ya Serikali ya Tanzania na Korea Kusini jana.

Akizungumza baada ya kusaini mkataba huo, Waziri wa Fedha, Mustafa Mkulo alisema fedha hizo zimetolewa kwa ajili ya kuunganisha umeme katika mikoa ya Iringa, Kigoma na Shinyanga pamoja na kuwekeza katika vifaa vya kisasa MUHAS.

Mkulo alisema katika fedha hizo, Sh bilioni 59.540 zimetengwa kwa ajili ya kuunganisha umeme katika mikoa hiyo na Sh bilioni 44.15 zimetengwa kwa awamu ya pili ya ujenzi wa chuo hicho pamoja na usambazaji wa vifaa vya hospitali.

Kwa upande wake, Mratibu wa Mradi wa Umeme, Makala Kingu alisema mradi huo utaanza baada ya kumaliza mambo mengi ambayo wahisani wanataka yakamilishwe.
“Baada ya mambo yanayohitajika kukamilika, ndio wahisani wataanza kutoa hizo fedha zao na sisi tunategemea kuyakamilisha Aprili mwaka kesho,” alisema.

No comments: