Mkuu wa mkoa wa Kigoma Luteni Kanali Mstaafu Issa Machibya ametembelea maeneo ya kijiji cha Munanila wilayani Kasulu na kijiji cha Mukarazi wilayani Kibondo vilivyopo mpakani mwa Tanzania na Burundi na kuvitaka vyombo vya ulinzi na usalama kuhakikisha kuwa hakuna uvunjaji wowote wa sheria unaotokea katika maeneo ya mpakani.
Mkuu huyo wa Mkoa wa Kigoma ameongeza kuwa wakati vyombo vya ulinzi na usalama vikiendelea kutekeleza majukumu yake hayo, nayo mamlaka ya mapato katika maeneo ya mpakani inatakiwa kusimamia kikamilifu ukusanyaji wa mapato kwa kutoza kodi bidhaa zote zinazostahili kutozwa kodi, iwe zinaingizwa nchini ama kwenda nchi jirani.
No comments:
Post a Comment