Karibu kwenye Blog ya Kijamii ya Kigoma yetu kwa habari na matangazo kwa bei nafuu sana. Tunakalibisha maoni, ushauri na habari zako ili tuijenge Tanzania kwa pamoja.

Thursday, October 6, 2011

Polisi wavuna mil 4.7 Kigoma

POLISI mkoani Kigoma imekusanya Sh milioni 4.7 kutokana na makosa mbalimbali yaliyofanywa na waendesha vyombo vya moto katika mwezi uliopita.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kigoma, Fraiser Kashai aliwaambia waandishi wa habari mwishoni mwa wiki iliyopita kwamba fedha hizo zilikusanywa kutokana na operesheni iliyofanywa na askari wa Usalama Barabarani.


Alisema yalibainika makosa 199 ambayo kati yake, 160 yalihusisha magari na makosa 39 yalihusisha pikipiki.


Alisema makosa 190 ndiyo yalilipishwa faini na mengine kushughulikiwa na na Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (Sumatra).


Akizungumzia Wiki ya Nenda kwa Usalama Barabarani iliyozinduliwa jana mjini hapa, Kamanda alisema zitafanyika shughuli mbalimbali hususan ukaguzi wa magari na pikipiki.


Aliwataka wamiliki wa vyombo vya moto kuvipeleka kukaguliwa ili vipewe stika maalumu. Alisema madereva watakaokaidi agizo watachukuliwa hatua.

No comments: