Karibu kwenye Blog ya Kijamii ya Kigoma yetu kwa habari na matangazo kwa bei nafuu sana. Tunakalibisha maoni, ushauri na habari zako ili tuijenge Tanzania kwa pamoja.

Tuesday, October 11, 2011

Kamati za Ukimwi lawamani Kigoma

KAMATI za Ukimwi za kata na vijiji katika Halmashauri ya Wilaya Kigoma, zimelaumiwa kwa kutotimiza majukumu yao katika kusimamia mapambano dhidi ya Ukimwi na kusababisha kuongezeka kwa maambukizi mapya.

Mratibu wa Ukimwi katika Sekretarieti ya Mkoa Kigoma, Badru Abdulnur alisema hayo mwishoni mwa wiki iliyopita katika mafunzo ya siku mbili kwa madiwani na maofisa watendaji

wa kata.

Mafunzo hayo yalihusu kuweka miundombinu ya pamoja ya washiriki hao katika kusimamia mapambano dhidi ya Ukimwi.


Abdulnur alisema viashiria vya kutotimiza wajibu wa watendaji hao ni pamoja na kuendelea kwa masoko ya usiku ambayo vikao mbalimbali vya kiserikali vimeshatoa agizo la kusimamishwa kwa masoko hayo.


Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya Kigoma, Adam Misana alisema kushindwa kuwepo kwa taarifa za watendaji hao katika masuala ya kupambana na Ukimwi, kunaonyesha jinsi gani viongozi hao walivyolipa kisogo jambo hilo.

No comments: