Karibu kwenye Blog ya Kijamii ya Kigoma yetu kwa habari na matangazo kwa bei nafuu sana. Tunakalibisha maoni, ushauri na habari zako ili tuijenge Tanzania kwa pamoja.

Saturday, October 22, 2011

Miradi ya mabilioni kuwekezwa Kigoma

KAMPUNI ya City Energy and Infrustructure ya Dubai, Falme za nchi za Kiarabu inatarajia
kuwekeza mtaji wa kiasi cha dola milioni 500 katika miradi mbalimbali ya maendeleo mkoani
Kigoma.

Hayo yalielezwa katika hafla ya kutia saini mkataba wa makubaliano kuhusu uwekezaji huo kati ya viongozi wa kampuni hiyo na uongozi wa Serikali ya Mkoa Kigoma.


Wakizungumza na waandishi wa habari baada ya kutia saini mkataba huo, viongozi wa Kampuni ya City Energy and Infrustructure walisema kuwa uwekezaji wao kwa sehemu kubwa

utajikita katika uchimbaji na usafishaji wa madini, uchimbaji wa makaa ya mawe na uzalishaji
wa umeme kutokana na makaa ya mawe na mabaki ya miwa.

Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni hiyo, Rajendra Patil alisema pia wanatarajia kujiingiza

katika kilimo cha mashamba makubwa ya miwa sambamba na uzalishaji wa sukari, kilimo cha
mashamba makubwa ya mahindi na uzalishaji wa bidhaa zitokanazo na mazao.

Alisema Tanzania ni nchi ya kwanza barani Afrika kwa kampuni hiyo kutaka kuwekeza kiasi

kikubwa cha fedha katika miradi mbalimbali na kwamba ujio wao nchini ulitokana na mkutano kati yao na Mbunge wa Jimbo la Kigoma Kaskazini, Kabwe Zitto ambaye aliwashawishi kuja
kuwekeza mkoani Kigoma.

No comments: