Karibu kwenye Blog ya Kijamii ya Kigoma yetu kwa habari na matangazo kwa bei nafuu sana. Tunakalibisha maoni, ushauri na habari zako ili tuijenge Tanzania kwa pamoja.

Tuesday, October 11, 2011

Makundi ndani ya CCM yakemewa Kigoma

CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Kasulu kimesema kuwa makundi yaliyokuwepo wakati wa uchaguzi mkuu uliopita, yameendelea kuwepo na kuathiri hali ya utendaji na
uimarishaji chama wilayani humo. Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Kasulu, Clement Ndayeza alisema hayo wakati akitoa taarifa ya hali ya maendeleo ya chama hicho wilayani humo kwa wanachama wa chama hicho.


Alisema kuwa hali ya utendaji ya chama na uhusiano imeendelea kuwa mbaya kutokana na

baadhi ya wagombea walioshindwa katika uchaguzi huo, kufanya mambo yanayokwamisha uimarishaji chama.

Kutokana na hilo, viongozi na watendaji wamekuwa wakitumia muda mwingi kusuluhisha migogoro baina yao na hali hiyo imegusa ngazi zote za chama kuanzia matawi hadi wilaya.


Mwenyekiti huyo alisema kikubwa kinachochangia kuwepo kwa jambo hilo ni kwa wagombea

walioshindwa kutotimiza majukumu yao kwa lengo la kukifanya chama hicho kiwe dhaifu
kwa sababu ya kutokuwepo kwenye uongozi.

Akizungumzia hali hiyo, Mjumbe wa Halmashauri Kuu (NEC) ya CCM Mkoa Kigoma, Christopher Chiza alisema kwa hali ya sasa ya chama, ni lazima mfumo mzima ubadilike na kurudi kule ambako Baba wa Taifa, Mwalimu Nyerere, alitaka chama kirudi.


Chiza alisema kuwa katika maeneo mengi chama kimekumbwa na hali hiyo na kuzorotesha

uhai wa chama na kwamba kwa hali ya sasa ya mfumo wa vyama vingi hali hiyo ni hatari katika mustakabali mzima wa chama hicho.

Alisema kuwa umasikini ndani ya chama pia unachangia baadhi ya wagombea wanaokuja

na fedha zao kutaka kuvuruga uamuzi na mfumo mzima wa chama.

Alisema ni lazima viongozi chama katika ngazi mbalimbali wabuni miradi ya kiuchumi

itakayowezesha chama kusimama imara bila kuwa ombaomba.

No comments: