Karibu kwenye Blog ya Kijamii ya Kigoma yetu kwa habari na matangazo kwa bei nafuu sana. Tunakalibisha maoni, ushauri na habari zako ili tuijenge Tanzania kwa pamoja.

Tuesday, October 4, 2011

Amuua mumewe kwa kuchoshwa na ulevi

JESHI la polisi mkoani Kigoma linamshikilia mkulima mmoja wa Kijiji cha Bukililo Wilaya ya
Kibondo mkoani Kigoma, Therezia Petro kwa tuhuma za mauaji ya mume wake baada ya kuchoshwa na ulevi wa kupindukia wa mwanaume huyo.

Kamanda wa Polisi mkoani Kigoma, Fraiser Kashai alisema mjini Kigoma kwamba mauaji hayo yalitokea mapema asubuhi juzi kijijini hapo na alimtaja marehemu aliyeuawa kuwa

ni Matata Ntoha Mkulima wa kijiji hicho.

Kamanda Kashai alisema kuwa kabla ya mauaji hayo ambapo mtuhumiwa

anadaiwa kutumia kitu chenye ncha kali wanandoa hao walianza kutupiana
maneno na sababu kubwa ikiwa ni ulevi wa mwanaume huyo ndipo mwanamke akachukua hatua ya kufanya kitendo hicho.

Baada ya mauaji hayo tukio hilo liliripotiwa katika kituo cha polisi wilayani Kibondo ambao walifika eneo la tukio na kumtia mbaroni mtuhumiwa ambaye anatarajia kufikishwa

mahakamani wiki ijayo kwa ajili ya kusomewa mashitaka yake.

Aidha, katika hatua nyingine Kamanda huyo wa Polisi amewashukuru wananchi mkoani humo kwa msaada mkubwa za taarifa za kuwepo kwa matukio ya uhalifu ambayo polisi walizifanyia kazi na kufanikiwa kuzima uhalifu huo.

No comments: