Karibu kwenye Blog ya Kijamii ya Kigoma yetu kwa habari na matangazo kwa bei nafuu sana. Tunakalibisha maoni, ushauri na habari zako ili tuijenge Tanzania kwa pamoja.

Thursday, September 29, 2011

Watendaji Kigoma kikwazo urejeshaji mikopo

MKUU wa wilaya Kigoma, John Mongela amesema , watendaji wa Idara ya Maendeleo ya Jamii katika Manispaa ya Kigoma Ujiji wamekuwa kikwazo katika kusimamia urejeshaji wa mikopo inayotolewa kwa vijana na wanawake kwa ajili ya kuanzisha miradi ya maendeleo.

Mongela alisema hayo katika kikao cha kamati ya ushauri ya mkoa wa Kigoma alipokuwa akihitimisha mjadala wa wajumbe wa kikao hicho waliokuwaa wakilalamikia kitendo cha halmashauri kutotenga fedha hizo za mikopo katika bajeti yake ya mwaka 2010/2011.


Alisema kuwa bado watendaji hao wa idara ya maendeleo ya jamii katika halmashauri hawajatimiza wajibu wao kikamilifu katika kuhakikisha mikopo iliyotolewa inarudishwa ili mfuko huo utune na kukopesha makundi mengine zaidi.


Alisema kuwa watendaji hao kwa kushirikiana na idara nyingine zinazohusika hususan Idara ya Fedha wanapaswa kukaa pamoja na kuweka mkakati wa ukusanyaji wa madeni hayo.


Akitoa maelezo ya sababu za kutotengwa kwa bajeti ya mikopo ya vijana na wanawake kaatika bajeti ya mwaka uliopita Mweka Hazina wa Manispaa ya Kigoma Ujiji, Livingstone Kahwa alisema kuwa inatokana na vikundi vilivyokopeshwa kutorejesha mikopo yao.


Kahwa alisema kuwa kutokana na kutorejeshwa kwa mikopo hiyo wameshachukua hatua ikiwemo kuwafikisha mahakamani baadhi ya wakopaji.


Alisema mwaka huu wa fedha manispaa imetenga asilimia 10 ya makusanyo yake ya ndani kwa ajili ya kutoa mikopo hiyo.


Akisoma taarifa ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo katika Manispaa hiyo Mkurugenzi Mtendaji wa Manispaa hiyo, Lewis Kalinjuna alisema kuwa Sh bilioni 14.7 zimepitishwa na bunge kwa ajili ya miradi ya maendeleo.

No comments: