MAJAMBAZI wawili wamekamatwa na Polisi mkoani Kigoma wakiwa na risasi 1,200 za silaha za kijeshi aina ya SMG wakizisafirisha kwenda Mpanda mkoani Rukwa.
Kaimu Kamanda wa Polisi mkoani Kigoma, Mrakibu Mwandamizi wa Polisi, Kihenya Kihenya, aliwataja watuhumiwa waliokamatwa wakiwa na risasi hizo kuwa ni Chamtu Tunugu (43) mkazi wa Kibande, Kasulu na Ismail Mateo (43) mkazi wa Mlole Kigoma Vijijini.
Kamanda Kihenya alisema watuhumiwa hao walikamatwa jana saa saba mchana kwenye Pori la Uvinza wakienda katika Pori la Mishamo wilayani Mpanda, maeneo wanayoishi wakimbizi wa Burundi.
Alisema askari Polisi wakiwa katika operesheni maalumu ya kupambana na uhalifu ukiwemo wa ujambazi wa kutumia silaha na wahamiaji haramu, walipata taarifa za kuwepo kwa watu hao katika pori hilo na hivyo na ndipo walipowaona na kufukuzana nao hadi kuwakamata na kiasi hicho cha risasi.
Hiyo ni mara ya tatu kwa Polisi mkoani Kigoma kukamata kiasi kikubwa cha risasi za bunduki za kijeshi aina ya SMG ambapo mara ya kwanza zilikamatwa risasi 1,858 na mara ya pili zilikamatwa 2,200 na kufanya risasi ambazo zimekwishakamatwa hadi sasa kufikia 5,258.
Kamanda huyo alisema Polisi wanaendelea na intelijensia kujua zinakotoka risasi hizo na watu wanaoziingiza na kwamba wanatafuta kujua mahala palipo na silaha zinazotumia risasi hizo.
Katika hatua nyingine, Polisi wa Kikosi cha Usalama Barabarani Kigoma wamekusanya zaidi ya Sh 810,000 katika siku mbili, Septemba 25 na 26 ikiwa ni makusanyo ya faini za papo kwa papo kwa madereva wasiozingatia taratibu, sheria na kanuni za usalama barabarani.
Jeshi la Polisi mkoani humo limeendelea kutoa mwito kwa kuendeleza juhudi za kuwafichua wahalifu ili wakamatwe na kukabiliana na mkono wa sheria.

No comments:
Post a Comment