Karibu kwenye Blog ya Kijamii ya Kigoma yetu kwa habari na matangazo kwa bei nafuu sana. Tunakalibisha maoni, ushauri na habari zako ili tuijenge Tanzania kwa pamoja.

Monday, September 26, 2011

Wakuu wa shule waambiwa wazingatie maadili Kigoma

WAKUU wa shule za sekondari mkoani K i g o m a wametakiwa kuzingatia maadili ya ufundishaji.

Ofisa Elimu katika Sekretarieti ya mkoa Kigoma, Floriana Ntikahavuye alisema hayo katika mahafali ya nne ya shule ya sekondari ya Mwilanvya wilayani Kasulu.

Alisema kuwa nidhamu mbovu ya wa nafunzi katika shule za sekondari ndiyo chanzo kikuu cha kuporomoka kwa taaluma.

Ntikahavuye ambaye alikuwa mgeni rasmi katika mahafali hayo alisema kuwa wakuu wa shule na bodi zao hawana budi kuwa wakali katika kuhakikisha wanafunzi wanakuwa na nidhamu ya hali ya juu.

Aliunga mkono kufukuzwa shule kwa wanafunzi kutokana na utovu wa nidhamu huku akitoa
mwito kwa wazazi kuzingatia jukumu la malezi bora kwa watoto wao.

Aidha ofisa elimu huyo aliipongeza shule hiyo kwa kufanya vizuri kitaaluma hali inayofanya wazazi wengi kuvutiwa kuwapeleka watoto wao.

Alisema changamoto katika elimu bado zipo siyo tu kwa shule binafsi bali pia za serikali ambazo zinaendelea kufanyiwa kazi.

Mkuu wa shule hiyo, Boniface Haramba aliwatupia lawama wazazi kwa kushindwa kusimamia nidhamu ya watoto wao hali inayoipa changamoto kubwa shule hiyo katika uendeshaji na kulazimika kuwafukuza wanafunzi wake wengi kila mwaka kwa utovu wa nidhamu.

Haramba alisema kuwa watoto wenye nidhamu nzuri wamekuwa na kiwango cha juu cha matokeo mazuri kitaaluma na hivyo kuchangia kuifanya shule hiyo kuendelea kufanya vizuri kitaaluma.

Wanafunzi 79 wanatarajia kuhitimu na uongozi wa shule umewahidi wanafunzi watakaofaulu kwa kiwango cha daraja la kwanza kwa alama kati ya saba na tisa kuwa watasomeshwa kidato cha tano na sita.
 
     

 

No comments: