Karibu kwenye Blog ya Kijamii ya Kigoma yetu kwa habari na matangazo kwa bei nafuu sana. Tunakalibisha maoni, ushauri na habari zako ili tuijenge Tanzania kwa pamoja.

Sunday, September 18, 2011

TASAF Kigoma yakomboa miradi 31

MFUKO wa Maendeleo ya Jamii (TASAF), umetumia Sh milioni 715 kwa ajili ya kumalizia miradi 31 ya kijamii katika Manispaa ya Kigoma Ujiji kutokana na kukwama kukamilika
kutokana na matatizo mbalimbali. 


Mratibu wa TASAF katika Manispaa ya Kigoma Ujiji, Staford Lilakoma aliwaambia hayo waandishi wa habari waliofanya ziara kutembelea miradi mbalimbali inayotekelezwa chini ya mfuko huo katika manispaa hiyo.

Alisema utekelezaji huo umefanyika katika madarasa 66 ya shule 17 za sekondari ambazo zilikuwa na upungufu mbalimbali.


Umefanyika ukarabati wa sakafu, dari , kuweka mtandao wa umeme na madirisha ya vioo .


Pia wamekamilisha ujenzi wa chumba cha kujifungulia katika zanahati ya Buhanda.


Lilakoma alisema kuwa wamelazimika kuomba fedha za ziada baada ya miradi mingi

kutekelezwa chini ya kiwango na kushindwa kukamilika.

Alisema wamelazimika kuwa na mhandisi wa ujenzi ambaye atakuwa akisimamia miradi ya

TASAF moja kwa moja na kutoa maelekezo katika ujenzi badala ya jukumu hilo kuachiwa kamati za utekelezaji miradi.

Mhakiki Rasilimali fedha wa miradi ya TASAF katika Manispaa ya Kigoma Ujiji, Haji Zaidi alisema kuwa katika fedha hizo, Sh milioni 650 zilikwenda moja kwa moja katika utekelezaji wa miradi, Sh milioni 9.7 kwa ajili ya posho za vikao za wajumbe wa kamati za miradi na Sh milioni 55 zilitumiwa na timu ya usimamizi ya miradi ya TASAF ya manispaa katika kusimamia shughuli za kila siku za miradi hiyo.


Akichangia kuhusu kukwama kwa miradi hiyo, Ofisa Mtendaji wa mtaa Mkese Kata ya Kagera

Manispaa ya Kigoma Ujiji, Havijawa Ndimuligo alisema kuwa uchangiaji wa asilimia 20 ya mradi ya nguvu za wananchi imekuwa chanzo cha kukwama kwa miradi hiyo kutokana na wananchi wengi kukataa kujitolea kuchangia.

No comments: