Karibu kwenye Blog ya Kijamii ya Kigoma yetu kwa habari na matangazo kwa bei nafuu sana. Tunakalibisha maoni, ushauri na habari zako ili tuijenge Tanzania kwa pamoja.

Saturday, September 3, 2011

Tanzania yasaili wakimbizi wa Kongo

Jumla ya watu 600 wanaokimbia kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, wanahifadhiwa kwenye kituo cha Nyarugusu mkoani Kigoma magharibi mwa Tanzania.

Wizara ya mambo ya ndani ya nchi inasema kwa sasa inawasaili watu hao kubaini wakimbizi wa kweli.

Kumekuwa na imani kuwa licha ya madai ya baadhi yao kukimbia vita maeneo ya Musisi na mengine kusini mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, wapo wanaokimbia tu makali ya maisha.

Nyarugusu ni kituo cha muda kwa wakimbizi wanaojiandaa kurejea makwao, na hivi sasa kinahifadhi wakimbizi 61,000 wakitunzwa kwa ushirikiano wa serikali na shirika la kimataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR.


No comments: