Karibu kwenye Blog ya Kijamii ya Kigoma yetu kwa habari na matangazo kwa bei nafuu sana. Tunakalibisha maoni, ushauri na habari zako ili tuijenge Tanzania kwa pamoja.

Saturday, September 3, 2011

Bomu lasalimishwa mkoani Kigoma“Tumeanza na mkakati wa muda mfupi ambao ni kukagua mabasi yaendayo sehemu mbalimbali nchini wakati yanaondoka na yanapofika huko yanakokwenda,” alisema Sirro na kuongeza;
“Lengo la ukaguzi huu ni kupunguza ajali na kuhakikisha kuwa madereva wanatambua kwamba lazima sheria zilizopo zifuatwe, hii ina maana kwamba hata askari wa usalama barabarani wataongezeka huku wakisaidiwa na kikosi cha farasi.”

Urudishwaji wa silaha
Katika hatua nyingine msemaji wa Jeshi hilo, Adivera Senso alisema tangu kuanza kwa operesheni ya kusalimisha silaha zinazomilikiwa na wananchi bila kibali, Julai 22, mwaka huu silaha 102 na bomu moja la kurusha kwa mkono zimesalimishwa.

“Silaha zilizohakikiwa ni SMG 26, Rifle 32, Shortgun 24, G3 moja, SAR moja, Gobore 16 na bomu moja,” alisema Senso nakuongeza; “Zoezi la kusalimisha silaha linafanyika katika ofisi za kata, wakuu wa wilaya au mkoa na silaha zinazomilikiwa kihalali zinatakiwa kupelekwa katika vituo hivyo kwa uhakiki mpya, zoezi hili limepewa miezi mitatu tu kuanzia Agosti Mosi mwaka huu.”

Alisema uwekaji wa alama silaha unaendelea katika Kanda Maalum ya Dar es Salaam na kwamba mpaka jana, jumla ya silaha 1,824 zilikuwa zimemeshawekewa alama.

Alisema mkoa unaoongoza kwa wananchi kusalimisha silaha hizo ni Rukwa ambako zimesalimishwa silaha 36 ukifuatiwa na Mkoa wa Mara ambako wananchi wamesalimisha silaha 15.“Dar es Salaam mpaka sasa zimesalimishwa silaha tano tu, ila bomu lilisalimishwa mkoani Kigoma,” alisema Senso.


No comments: