RAIS Jakaya Kikwete, leo anatarajiwa kufungua mkutano wa wakandarasi na wadau wengine wa sekta ya ujenzi utakaofanyika jijini Dar es Salaam.
Mkutano huo wa siku mbili, ni mwendelezo kusherekea miaka 50 ya uhuru wa Tanganyika, kwa Wizara ya Ujenzi ambayo ilianza kusherekea maadhisho hayo Septemba mosi mwaka huu.
Mkutano huo utakaofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Mlimani City, utajadili masuala mbalimbali yanayohusu sekta hiyo muhimu katika maendeleo ya nchi.

Akizungumzia mkutano huo, Msajili wa Bodi ya Wakandarasi (CRB, Boniface Muhegi, alisema utahudhuriwa na wadau 1,500 na kwamba baadhi yao watatoka nje ya nchi.
Alizitaja nchi zitakazokuwa na uwakilishi kuwa ni pamoja na Kenya, Malawi, Zambia na Afrika Kusini.
Msajili huyo alisema wageni katika mkutano huo ni pamoja na Katibu Mkuu wa Wizara ya Barabara wa Kenya, Michael Kamau.
Waziri wa Ujenzi, Dk Ujenzi John Magufuli, alisema katika mkutano huo washiriki watapewa fursa ya kuzungumza mambo mbalimbali yanayohusu sekta ya ujenzi hasa wa barabara.
“Pia washiriki katika mkutano huo watapata fursa ya kutoa ushauri wa nini kifanyike katika kipindi cha miaka 50 ijayo,”alisema Dk Magufuli
Katika mazungumzo yake, waziri huyo alisema kuanzishwa kwa Wkala wa Barabara Nchini (Tandroads) ni moja ya mafanikio makubwa katika sekta hiyo.
Kwa mujibu wa Dk Magofuli Tanroads ambayo imekuwa na jukumu la kusimamia miradi ya barabara hapa nchini, ilianzishwa chini ya sheria namba 30 ya mwaka 1970.
No comments:
Post a Comment