Karibu kwenye Blog ya Kijamii ya Kigoma yetu kwa habari na matangazo kwa bei nafuu sana. Tunakalibisha maoni, ushauri na habari zako ili tuijenge Tanzania kwa pamoja.

Friday, August 26, 2011

Serikali yawatupia jicho wavuvi Rukwa, Kigoma


NAIBU Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi, Benedict ole Nangoro, amesema Serikali katika mwaka huu wa fedha itaanzisha miradi midogo ya kuwezesha wavuvi katika mikoa ya Rukwa na Kigoma, ili kuondokana na umasikini.

Alisema hayo bungeni wakati akijibu swali la Mbunge wa Nkasi Kusini, Desderious Mipata (CCM), aliyetaka kujua Serikali ina mpango gani wa haraka wa kuwanusuru kiuchumi
wananchi wa jimbo hilo ambao ni masikini kwa sababu ya kutumia zana duni za usafiri na uvuvi.

Mbunge huyo pia alihoji endapo Serikali inakubaliana na ushauri kuwa wananchi hao wauziwe vyombo vya uvuvi kama njia mojawapo ya kunusuru tatizo la umasikini hasa
katika kata za Wampembe, Kala na Ninde.

Akijibu maswali hayo, Ole Nangoro alisema Serikali itawezesha wananchi hao kupitia Mradi
wa Uwiano wa Usimamizi wa Mazingira ya Bonde la Ziwa Tanyanyika chini ya uratibu wa
Ofisi ya Makamu wa Rais.

Ole Nangoro alisema ili kutekeleza hilo, Euro 480,000 zimetengwa kwa ajili ya kuanzisha miradi mbalimbali ikiwemo ya uvuvi na utunzaji wa mazingira.

Alisema pia Serikali imeondoa ushuru wa zana za uvuvi, vifaa vinavyotumika kutengeneza
nyavu, injini za kupachika pamoja na vifungashio vya mazao ya uvuvi zinazoingizwa
nchini, ili kupunguza bei ya vifaa hivyo na hivyo kuwapa wavuvi unafuu wa bei.

No comments: