Karibu kwenye Blog ya Kijamii ya Kigoma yetu kwa habari na matangazo kwa bei nafuu sana. Tunakalibisha maoni, ushauri na habari zako ili tuijenge Tanzania kwa pamoja.

Friday, September 2, 2011

Waziri Huvisa auagiza uongozi manispaa ya ujiji kurekebisha kasoro ujenzi wa madarasa


Waziri wa nchi ofisi ya makamu wa rais Mazingira Dkt. Terezya Huvisa ameuagiza uongozi wa Manispaa ya Kigoma Ujiji na wataalam wake, kurekebisha mara moja kasoro zilizopo katika madarasa mawili yaliyopo katika shule ya msingi Bangwe, ambayo yamejengwa chini ya ufadhili wa mradi wa kuhifadhi Mazingira ya Ziwa Tanganyika.
Dakita Huvisa ametoa agizo hilo kufuatia  kuta na sakafu za madarasa hayo, kuanza kupasuka kabla hata hayajaanza kutumika na kwamba uongozi wa Manispaa hiyo na wataalam wake, upaswa kuhakikisha kuwa ukamilishaji wa ujenzi wa wodi ya wazazi iliyopo Katonga na vyoo vilivyopo eneo la Kibirizi mjni Kigoma unakidhi viwango vinavyotakiwa.
Katika ziara yake, Dakita Huvisa amekagua pia Visima vya maji vilivyopo Katonga na Bushabani, mradi wa madarasa mawili ya shule ya Msingi Kieba  pamoja na ujenzi wa vyoo eneo la Kibirizi, ambavyo pamoja na kasoro za hapa na pale lakini ameridhishwa na ujenzi wake.

No comments: