Karibu kwenye Blog ya Kijamii ya Kigoma yetu kwa habari na matangazo kwa bei nafuu sana. Tunakalibisha maoni, ushauri na habari zako ili tuijenge Tanzania kwa pamoja.

Wednesday, August 24, 2011

Familia ya Nyerere imetelekezwa, na hii ni aibu kubwa, hivi Serikali hailioni hata hili?

Hayati Baba wa Taifa Mwl Nyerere


“Familia ya Nyerere imetelekezwa, na hii ni aibu kubwa, hivi Serikali hailioni hata hili? Ni
lini itasikia kilio cha Watanzania?

Kama imeshindwa kuhakikisha maji yanapatikana kwa familia ya Nyerere, vipi kwa familia ya Kigwangalla isiyofahamika?” Alihoji.

Dk. Kigwangalla alikuwa akichangia hoja kuhusu Makadirio ya Matumizi ya Wizara ya Maji kwa mwaka 2011/12 iliyowasilishwa bungeni juzi na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Uhusiano na Uratibu, Stephen Wasira.

Wasira aliwasilisha hoja hiyo kutokana na Waziri wa Maji Profesa Mark Mwandosya, kuwa India kwa matibabu kwa zaidi ya wiki tatu sasa.

Akichangia Dk. Kigwangalla alisema haungi mkono hoja kwa kuwa suala la maji limekuwa kero kubwa si kwa wananchi wa chini peke yao lakini hata kwa watu muhimu kwa Taifa kama familia ya Mwalimu Nyerere na kuitaka Serikali kutoa majibu kuhusu adha hiyo.

Kuhusu jimboni kwake, alisema: “Naogopa kuonekana punguani au mwehu na wajukuu zangu kama nikiunga mkono hoja hii, kwa kuwa asilimia 63 ya wananchi wa Nzega hawana maji, hatuelewi msamiati wa mtaalamu mwelekezi, huu msamiati ubadilike jamani”.

Kwa upande wake, Mkono aliitaka Serikali kumwondoa mara moja wizarani, Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji, Christopher Sayi, kwa kuwa hana msaada wowote wa kufumbua tatizo la maji, bali anachekacheka tu; akataka mradi wa Butiama ushughulikiwe haraka ili mjane wa Mwalimu, Mama Maria apate maji.

“Siungi mkono hoja mpaka nielezwe wananchi wa Musoma Vijijini watapata maji lini, kuna huu mradi mkubwa wa kitaifa wa mpaka Butiama tangu mwaka 1974, sasa umesahaulika
kabisa, Mama Maria pale hana maji, kijiji cha Kyabakari maji hakuna, wafanyakazi wa mradi huu hawalipwi mshahara miaka kadhaa sasa, tunakwenda wapi?” Alihoji Mkono na kuongeza:

“Kuna shida kuanzia serikalini, fedha zikitolewa haziwafikii walengwa, ni kama Serikali ya Musoma Vijijini haipo miaka 10. Siungi mkono mpaka kieleweke, kuna mtu anaitwa Sayi hapo wizarani, anachekacheka tu, sijui anasubiri nini hapo, aondolewe maana hana kitu alichofanya tangu hata kabla hajawa Katibu Mkuu mpaka leo.”

No comments: