Karibu kwenye Blog ya Kijamii ya Kigoma yetu kwa habari na matangazo kwa bei nafuu sana. Tunakalibisha maoni, ushauri na habari zako ili tuijenge Tanzania kwa pamoja.

Sunday, February 3, 2013

SHEREHE ZA MIAKA 36 YA CCM ZAFANA MKOANI KIGOMA 2013

Mwenyekiti wa CCM Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiingia uwanja wa Lake Tanganyika kuhitimisha sherehe za miaka 36 ya chama hicho mjini Kigoma leo 
 Ngoma za utamaduni zamfurahisha  Mwenyekiti wa CCM Rais Jakaya Mrisho Kikwete
Licha ya vyombo kukorofisha msanii Diamond nma kundi lake walitumbuiza kwa ustadi
 Akipungia kwa furaha maelfu ya wananchi wa Kigoma wanaomshangilia kwa nguvu
 Diamond akipagawisha

Katibu Mkuu wa CCM,Ndg. Abdulrahman Kinana akisema machache,muda mfupi kabla ya kumkaribisha Mwenyekiti wa CCM,Rais Jakaya Mrisho Kikwete (hayupo pichani} kuwahutubia wananchi wa Mkoa wa Kigoma jioni hii.
Waziri wa Uchukuzi,Dkt. Harisson Mwakyembe akiwahutubia wananchi wa Mkoa wa Kigoma jioni hii na kuwahakikishia kuwa sasa hivi mkoa wa Kigoma mambo yako vyema kabisa na treni itaendelea kufanyaka kazi kama zamani.
Mwenyekiti wa CCM Rais Janakaya Kikwete akiongoza matembezi ya maadhimisho ya miaka 36 ya CCM, leo asubuhi kutoka eneo la Mnarani hadi ofisi ya CCM mkoa wa Kigoma leo. Wengine ni Makamu Mwenyekiti wa CCM (Bara) Philip Mangula, Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Kigoma Dk. Amani Kaborou, Mama Salma Kikwete, Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana na Katibu wa NEC Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Dk. Asha-Rose Migiro (kulia)
Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete na Mama Salma Kikwete wakiongoza matembezi ya mshikamano ya Miaka 36 ya CCM, mjini Kigoma leo
Matembezi hayo yakipita eneo la Burega, Barabara ya Kigoma-Ujiji
Mwenyekiti wa CCM, Rais Kikweye akiwa na muaasisi mmoja wa CCM ( ambaye jina lake halikuweza kupatikana mara moja) baada ya matembezi kufika Ofisi ya CCM mkoa wa Kigoma
"NDUGU WANANCHI, NAWAPONGEZA KWA KUSHIRIKI KWA WINGI KWENYE MATEMBEZI HAYA. HAPA SISEMI MENGI TUKUTANE MCHANA PALE UWANJA WA LAKE TANGANYIKA" Akasema Rais Kikwete wakati akizungumza na wananchi baada ya matembezi hayo

No comments: