
Tawi hilo jipya litakuwa la
23 nchi nzima huku benki hiyo ikiwa imethubutu kufungua matawi mengine mawili
nje ya nchi yakiwa nchini Comoro na Djibouti.
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa tawi hilo, Mkurugenzi wa
benki hiyo, Hanif Jaffer, alisema ufunguzi wa tawi hilo ni utekelezaji wa
mpango wa benki unaolenga kuhakikishia wananchi wengi wanapata huduma bora za
kibenki.
Jaffer alisema benki yake imeamua kufungua tawi hilo kutokana na ukweli kuwa Mkoa wa Kigoma ni kiungo
muhimu kwa wananchi wanaofanya biashara na nchi jirani za Burundi na
Jamhuri ya Demokrasia ya Kongo.
Alisema kuwa benki yake itaendelea kuwapatia wajasiriamali
wadogo na wakati uwezo wa kifedha ili kuwasaidia kupanua biashara zao.
“Jitihada zetu ni kuhakikisha tunafikia wananchi wengi
waliopo pembezoni. Tuna imani kuwa ufunguzi wa tawi letu jipya hapa litasaidia
kupunguza tatizo hilo,”
alisema Jaffer.
No comments:
Post a Comment