Karibu kwenye Blog ya Kijamii ya Kigoma yetu kwa habari na matangazo kwa bei nafuu sana. Tunakalibisha maoni, ushauri na habari zako ili tuijenge Tanzania kwa pamoja.

Saturday, April 21, 2012

Polisi Kigoma yaanza kuchunguza mauaji

 Kigoma mjini

JESHI la Polisi mkoani hapa limeanza uchunguzi wa mauaji ya watu wanne yakiwemo ya mkazi mmoja wa kijiji cha Muhange Wilaya ya Kibondo mkoani humo Misigalo Kamoli (53).

Kamoli alikutwa ameuawa juzi shambani kwa mkazi mmoja wa kijiji hicho baada ya kushambuliwa na watu wasiojulikana. Mauaji mengine ni ya wale waliotuhumiwa kujihusisha na uchawi.

Kamanda wa Polisi mkoani Kigoma Kamishna Msaidizi Frasser Kashai, alisema mwili wa marehemu ulikutwa ukiwa na jeraha la kuchomwa na kitu chenye ncha kali sehemu ya kwapa la mkono wa kushoto.

Kamanda Kashai alisema pamoja na kuwa Polisi wanaendelea na uchunguzi juu ya tukio hilo, huenda marehemu alishambuliwa na watu baada ya kukurupushwa nyakati za usiku kijijini hapo.

Alisema kumbukumbu za Polisi zinaonesha kuwa mwaka 2009 marehemu Misigalo aliwahi kuhukumiwa kifungo cha mwaka mmoja gerezani kwa kosa la kuvunja nyumba usiku na kuiba.

Wiki iliyopita Jeshi la Polisi mkoani Kigoma liliwakamata watu wanane kwa tuhuma za kuhusika na mauaji ya watu watatu kwa kisingizio cha hasira kali.Watu wawili

No comments: