Karibu kwenye Blog ya Kijamii ya Kigoma yetu kwa habari na matangazo kwa bei nafuu sana. Tunakalibisha maoni, ushauri na habari zako ili tuijenge Tanzania kwa pamoja.

Wednesday, February 8, 2012

Polisi yasaidiwa kompyuta kupambana na uhalifu mipakani Kigoma

SHIRIKA la Umoja wa Mataifa linalohusika na Uhamiaji (IOM), limetoa msaada wa kompyuta
sita kwa Jeshi la Polisi Mkoa wa Kigoma, ili kuimarisha utendaji kazi wake wa kupambana na vitendo vya uhalifu kwenye mipaka yake.

Akizungumza na waandishi wa habari baada ya kupokea vitendea kazi hivyo mwishoni mwa wiki, Kamanda wa Polisi wa Mkoa, Fraiser Kashai alisema vitasaidia katika kuimarisha hali ya ulinzi na usalama mkoani humo.


Kamanda Kashai alisema wakati huu wa zama za sayansi na teknolojia kuwepo kwa vitendea kazi hivyo kunawafanya wote wanaohusika na ulinzi na usalama kwa wananchi na mali zao kufanya kazi kama timu moja.


Alisema kompyuta hizo zitakazotumika kuwafundisha maofisa wa Polisi na Idara ya Uhamiaji zitaunganishwa pia na mtandao, zitakuwa msaada mkubwa katika kupata habari mbalimbali zikiwemo za wahamiaji haramu.


Akizungumzia kuhusu vifaa hivyo, Ofisa Miradi wa IOM, Marcelino Rumkishun alisema kompyuta hizo zina thamani ya Sh milioni 10 na ni sehemu ya mkakati wa shirika hilo katika kuisaidia mikoa minne ya Kanda ya Magharibi na Ziwa katika kupambana na vitendo vya uhamiaji haramu na wahalifu.

1 comment:

Anonymous said...

Ni suala zuri kiusalama ingawa nastaajabu hao jamaa wa IOM wanapaswa pia kusaidia kuinua hali ya uchumi wa wananchi wanaoishi mikoa kama Kigoma ambao kwa muda mrefu imekuwa ni kimbilio la wakimbizi hivyo pamoja na kusapoti suala la usalama lakini pia wasapoti na miradi ya kijamii na kiuchumi ili kuwasaidia watu wa kigoma ambao wamedhoofishwa sana na uwepo wa wakimbizi ktk maeneo yao