Karibu kwenye Blog ya Kijamii ya Kigoma yetu kwa habari na matangazo kwa bei nafuu sana. Tunakalibisha maoni, ushauri na habari zako ili tuijenge Tanzania kwa pamoja.

Thursday, December 8, 2011

Wanaokwepa kodi kushitakiwa, Kigoma

MAMLAKA ya Mapato (TRA) mkoani Kigoma inakusudia kuwafungulia mashitaka wafanyabiashara wote mkoani humo wanaokwepa kulipa kodi zao kwa mujibu wa sheria.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa maadhimisho ya Wiki ya Mlipa Kodi, Meneja wa TRA

mkoani hapa, Ernest Dundee alisema mamlaka yake imeamua kuchukua hatua hiyo, baada ya wafanyabiashara kwa makusudi kukwepakulipa kodi za biashara zao.

Alisema kuwa licha ya mafanikio ya kuongezeka kwa makusanyo ya Sh bilioni 1,03 sawa na asilimia 20 ya ongezeko kutoka mwaka wa fedha 2009/2010, bado wafanyabiashara wengi huingiza bidhaa zao ndani ya nchi kwa magendo kwa nia ya kukwepa kodi.


Alisema makusanyo ya kodi yameongezeka kutoka wastani wa Sh milioni 436.2 kwa mwezi kutoka mwaka 2009/10 na kufikia wastani wa Sh milioni 485.5 kwa mwezi kwa mwaka 2010/11 ongezeko la wastani wa Sh milioni 49.2 sawa na asilimia 11.2.

No comments: